NAJUTA KUZALIWA MWANAMKE 11
MTUNZI ,J.J
Jesca akiwa uchi wa mnyama alibebwa na kupelekwa chumba cha adhabu
Alifungwa mikono na miguu kisha alitundikwa juu kabisa na chini yake waliweka makaa ya moto hivyo miale ya moto ilikua ikimfikia jesca
Hakika adhabu hii ilikua ni kubwa sana kwa jesca ukitegemea alikua na majeraha ya pasi mgongoni
Jesca alipiga kelele kwa uchungu sana
Alibanikwa ka mshikaki ,alijigeuza na kujipindisha kukwepa miale ile ila maumivu yalikua palepale
Alilia sana ,,,mama shushu alimsogelea na kumwambia
``umesahau ulisema kwenye gari ni bora mniue ,ndio nakuua sasa’’
Jesca alipiga kelele kwa nguvu ``mama nipige hata bunduki nife siwezi stahimili kifo hiki ‘’
Zilipopita dakika kumi jesca akiwa kwenye mateso ,maumivu yalimzidi hadi alipoteza fahamu
Masoye kijana wa kazi alikata kamba ile kwa ajili ya kumsaidia jesca
Alivyoikata kamba mama shushu na yeye alitokeza
``MHHHH MASOYA unampeleka wapi huyu????’’
``Mama shushu hamna namna huyu atakufa mama nimeona nimtoe jamaniiii’’
``ok masoya ila jitahidi sikunyingine ukirudia kosa kama hili tusionane wabaya maana nimepanga hivi wewe unafanya kinyume ‘’
Jesca alirudishwa kwa wadada makahaba alipelekwa bafuni aliogeshwa ,kisha alifungwa vizuri majeraha yake,,,,,,,Akiwa anaogeshwa na dada mmoja ,dada huyo alimsemesha
``sikia mdogo angu ukiwa chini ya himaya hii tambua kuwa wewe si mali yako wewe ni cha wote sawa??? Kubali kutumika lasivyo hapa utauawa tu hamna namna ,wapo wasichana wengi waliosimamia misimamo yao kilichowakuta ni kifo sawa ???’’
Jesca alitikisa kichwa ishara ya kumsikia ,hakutaka kuongea mengi jesca alikua ameshajikatia tamaa alikua tayari kufa kabisa
Baada ya kuanyiwa usafi alipelekwa katika chumba Fulani ,hakika chumba hiki kilivutia sana ,jesca aliwekwa humo ,akiwa amepumzika katika kitanda cha chumba hicho alikuja bibi m,moja na kwenda moja kwa moja hadi alipo jesca
``mwanangu hujambo nimeambiwa una majeraha mgongoni nimekuja kukutibu kama nilivyoagizwa ‘’
Jesca bila kubisha alijigeuza ili kumpa bibi huyo nafasi ya kuweza kumtibu ,bibi Yule alipoyaangalia majeraha ya jesca kwa mshangao alimuuliza
``duuuu mwanangu nini kilikukuta mbona kama moto huu jamanii’’
``ndio bibi nilichomwa na pasi ‘’
Bibi Yule alijikuta akitokwa na machozi huku akisema ``bila shaka mtu aliyefanya unyama kama huu lazima atakufa tu’’
Jesca alijibu ``walionifanyia hivi washalipwa yao bibi washakufa’’
Bibi Yule alikuja na asali akapaka kwenye vidonda vya jesca
Baada ya wiki moja vidonda vya jesca vilifunga kabisa alikua mzima ,alirudia hali yake ya mwazo
Mama shushu alifurahi sana alijisemea
``sasa ni muda wa kupiga hela huyu mtoto mzuri sana ,hapa maskini hasogelei ,mtu akija na laki au elfu hamsini ruksa kulala nae ‘’
Jesca alikua bomba sana alipambwa akapambika siku hiyo kwa ajili ya kazi
Ilipofika majira ya saa saba ,,,walikuja matajiri kibao katika kambi ile
Mama shushu akiwa kifua mbele aliwaingiza matajiri wale kwa ajili ya kuchagua vimwana wa kujiliwaza nao
Zaidi ya matajiri watano walimchagua jesca kila mmoja alitamani kulala na jesca ,sasa ilifika wakati sasa atakaye panda dau kubwa ndio apewe
Wa kwanza alisema laki wa pili laki tatu ,watatu alisema laki nne aliyevunja rekodi alisema atatoa laki saba alale na jesca usiku mmoja
Mama shushu alifurahi sana ,,,,,,alimvuta jesca pembeni na kumwambia
``unaona ulivyo mrembo tumika vizuri nitakupa zawadi kesho sawa????’’
Jesca akiwa anaongea na mama shushu kichefuchefu kilimshika akatapika hapo hapo ,ikumbukwe jesca alikua na ujauzito wa hussein ,kutokana na hali ile hadi kichanga kilichomo tumboni kilichukia
Mama shushu kwa panic aliuliza
``wewe jesca usikute wewe ni mjamzito eee’’
Kwa haraka alichukuliwa na kupelekwa kufanyiwa vipimo
Ndani ya dakika mbili aliyemfanyia vipimo alipeleka majibu kuwa jesca anaujauzito wa miezi miwili na nusu
Mama shushu alihisi kuchanganyikiwa alisikia hasira sana kwa haraka aliagiza jesca apelekwe chumba cha kutolea mimba na mimba ile itolewe
Jesca alisikia yote ,,,jesca alikumbuka sana maneno ya bwana ake Hussein ``mke wangu nitunzie kichanga na pindi akizaliwa mpe jina happy yaan furaha ya ulimwengu ;’’
Jesca alipokumbuka maneno hayo alisema kwa nguvu
``hamwezi kutoa mimba yangu kuliko mnitoe bora mniuwe sipooooo tayari’’
Mama shushu alifikishiwa taarifa hizi ,kwa hasira alikuja akiwa anahema sana ,kila aliyemwona alijua hapa kuna mtu anakufa
Nini kitaendelea ……………………………
No comments