NAJUTA KUZALIWA MWANAMKE 10
MTUNZI :Joshua shao
Akiwa anaondoka ,cathe aliingia chumbani kwa haraka alipiga mkono kwenye begi lake alitoa picha moja ambayo walipiga siku ya sherehe ilikua ni picha ya Hussein akiwa jesca pia alitoa picha moja akiwa Hussein peke yake
Cathe alimkimbilia jesca kwa bahati nzuri alimwona kwa mbali aliita
``jescaaaaaa’’
Jesca alisubiri
Cathe alianza ``wifi nisamehe tambua mimi siko upande wa hawa jamani nakupenda sana ila sina namna ya kukusaidia my dia ,nimekuletea hizi picha zitakuwa kama kumbukumbu kwako’’
Jesca alipokea picha zile alipotazama picha aliyopiga na hussein machozi yalimtoka upya
Jesca alimshukuru sana cathe na kumwahidi kuwa ipo siku
Cathe alimpatia jesca shilingi elfu tano na kumwambia
``wifi sina chochote ila hii itaweza kukufaa japo hata chai’’
Jesca alimkumbatia wifi ake kisha waliagana
Cathe alisikia uchungu sana ila hakuwa na namna
Jesca alianza kukata mtaa asijuwe wapi wanaenda
Akiwa anatembea kwa mbali aliona gari jeusi ,moyo wake uloigonga
``Paaaaaaa’’ kwani gari lile limefanana kabisa na gari la mama chuchu aliyemteka kipindi kile
Jesca akiwa anashangaa taratibu gari lilisogea karibu kabisa na yeye kama vile linamfuatilia
Jesca moyo wake ulimpasuka
``paaaah!!!!!!!!!!!! ‘’ alihisi hali ya hatari alijua leo wenda akakamatika ,jesca alihaha huku na kule alikimbia asijue anakimbilia wapi
Akiwa anababaika dereva Yule alikata kona kiufundi sana na kumtega jesca kwa mbele
Kisha vioo vilishushwa na wao walishuka
Jesca kutokana na masahibu yaliyomkuta alikua mchovu alitamani kunyanyua mguu wake akimbie ila alikua amechelewa na hata kama angekimbia lazima tu angedakwa asingefika mbali
Walishuka vijana wawili wakiwa wamejifunika usoni kwa kitambaa ,,,,sura zao zilikuwa hazionekani ,walimfuatilia jesca kisha walimshika ,kila mmoja alishikilia bega lake ,,na mmoja alisema kwa nguvu
``mama shushu huyu binti ndio Yule ‘’
Mama shushu mkuu wa kambi ya makahaba alishuka kwa maringo huku akicheka kicheko cha dharau sana
``hahahahah kwa hiyo ulidhani ungefanikiwa kunikimbia mimi hahahahaahah mimi ndio mama shushu jiji zima linanijua ,sasa wewe unatoroka kambi unadhani utakuwa salama ‘’
Mama shushu alizishika nywele za jesca mithili ya mtu anachuma mboga ,alizivuta na kuzining’iniza huku akisema
``mwaruni huyu tumuue ama tumpeleke kambini ,kwa sasa kadhohofu sana atafaa kwa kazi ‘’
Mwaruni kijana wa kazi wa mama shushu alijibu
``mkuu wangu huyu bado anafaa kwa matumizi naona sura inalipa mama ake hapa huyututapiga hela ‘’
Mama shushu alisema
``hapana huyu mimi naona tumuulie hapa alisababisha mengi sana baada ya kuamua kutoroka ,tulipoteza maisha ya walinzi wengi si tu walinzi nilipoteza hela nyingi sana’’
Masoya kijana alikurupuka na kusema
``kwahiyo mama huyu tumuue siyo ‘’
``yeaah mnaweza kumuua ‘’
Walinyanyua visu vyao tayari kummalizia, jesca lakini kabla hawajafanya hivyo mama shushu alisema
``stooooooop,wacha kamateni huyu twende nae ‘’
Jesca alishikwa na kutupwa ndani tayari kurudishwa kambi aliyoikimbia kwa gharama kubwa
Jesca akiwa ndani ya gari lile alisema
``eee Mungu nimekukosea nini mimi mpaka mambo kama haya yananikuta mja wako ,’’
Jesca alikua akilia sana ila ndani ya gari hakuna aliyekuwa akimsikiliza hata kidogo mama shushu alikua akiendelea kuongea na masoya
``unajua masoya ile kambi yetu ulinzi unapaswa kuimarishwa sana hakuna upuzi kama kutoroka kambi ‘’
``ni kweli mama shushu mimi naona pia ziwekwe adhabu kali ili kuwavunja moyo watorokaji,yaan mtu akitaka kutoroka akishikwa apewe adhabu ya kifo kabisa hii ndilo suluhisho ‘’
``kweli masoya umeonea point muhimu sana kwa sasa hatutruhusu uzembe adhabu mara zote tumezoea kuwapa nwalinzi wasa hivi wote wanapata adhabu na leo naenda kuwatangazia kabisa ili kila mtu atambue ,,,,,mimi nashangaa kama mtu umeletwa pale kazi yako kuhudumia wateja kuna shida gani kwani ungekua umeolewa si ungempa mumeo kwani ukiuzia wanaume wengine kuna shida gani chakula tunakupa nguo tunakupa chakula khaaa ya nini kukimbia ‘’
Jesca akiwa ndani ya gari aliyasikia yote aliendelea kulia kwa kwiki huku akiongea kwa uchungu sana
``nimekosea nini mimi ,nimekosea nini ,,,’’
Mama shushu alimzaba jesca kofi la nguvu
``paaah unalia nini nyambafu wewe hapa bado hujaianza adhabu yako ,nimekusamehe kifo unaleta utani’’
Jesca alikua na hasira sana aliropoka kwa nguvu
``kama vipi niueni tu sioni umuhimu wa kuishi’’
Lilikua ni kosa kubwa sana kwa jesca laity kama angejua akanyamaza kimya waswahili wana sema ``hasira hasara ‘’
Hatimaye waliingia katika kambi ile
Jesca kwa mara nyingine tena aliweza kuona mazingira aliyoyakimbia kipindi kile
Sauti ilisikika ``mwingizeni ndani huyu ‘’
Jesca alibebwa na kupelekwa ndani ya chumba Fulani
Sehemu ya kuuzia makahaba kulikua na wakina dada wengi makahaba waliobobea ambao walikua wakifundisha wenzao ,mienendo na mapozi ya kikahaba
Jesca aliletwa alivyoingizwa ndani kila mmoja alipiga kelele
``uwiiiiiiii mama shushu huyu cute umemleta wapi hakika huyu ndio mrembo wa kambi yetu ,haki hakuna binti mrembo ka huyu ‘’
Mama shushu alijibu
``mpeni mazoezi huyu natamani leo niingize pesa nyingi kwa ajili yake ‘’
Jesca aliamriwa na mkuu wa makahaba kuvua nguo zake zote
Jesca hakupinga alifanya hivyo
Makahaba walimpigia makofi kwani alikua na mwili wa mvuto sana ila mmoja alionekana akisikitika
Wenzake walimuuliza
``mbona una nuna shanifa kuna tatizo???’’
``ndio mama shushu huyu ana jeraha kubwa mgongoni amedhurika tayari sijui kama atafaa kivile ‘’
``kila mtu alimgeukia jesca na kumtazama ‘’
Maskini kila mmoja alitokwa na chozi isipokuwa mkuu wao mama shushu
Kutokana na kuburuzwa na watekaji jesca alivitonesha vidonda vyake ,,,,kama mnavyokumbuka jesca aliwahi kuchomwa na pasi ya moto na mama kenedy ,alipokuwa akikokotwa kwenye gari alivitonesha sana
Mama shushu aliuliza kwa hasira
``haya hii midonda umetoa wapi wewe ,si ulikua mzima ‘’
Jesca hakujibu kitu alimtazama mama shushu tu usoni ‘’
``hujibu siyo hahahahah ‘’ mama shushu alicheka kwa kejeli
Haya kamateni huyu mpeleke chumba cha mateso naona analeta masihara
Kahaba mmoja alimwonea sana jesca huruma alisema
``Ila mama shushu ungemwacha afanyiwe matibabu ndani ya siku tatu atakuwa sawa tu mbona ‘’
Mama shushu alisema
``naona mnakiuka masharti yangu kamateni pelekeni chumba cha mateso ‘’
Jesca akiwa uchi wa mnyama alibebwa na kupelekwa chumba cha adhabu
Alifungwa mikono na miguu kisha alitundikwa juu kabisa na chini yake waliweka makaa ya moto hivyo miale ya moto ilikua ikimfikia jesca
Hakika adhabu hii ilikua ni kubwa sana kwa jesca ukitegemea alikua na majeraha ya pasi mgongoni
Jesca alipiga kelele kwa uchungu sana
Alibanikwa ka mshikaki ,alijigeuza na kujipindisha kukwepa miale ile ila maumivu yalikua palepale
Alilia sana ,,,mama shushu alimsogelea na kumwambia
``umesahau ulisema kwenye gari ni bora mniue ,ndio nakuua sasa’’
Jesca alipiga kelele kwa nguvu ``mama nipige hata bunduki nife siwezi stahimili kifo hiki ‘’
Zilipopita dakika kumi jesca akiwa kwenye mateso ,maumivu yalimzidi hadi alipoteza fahamu
Masoye kijana wa kazi alikata kamba ile kwa ajili ya kumsaidia jesca
Alivyoikata kamba mama shushu nay eye alitokeza
Je nini kitaendeleaa
Maskini jesca ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,fuatilia mkasa huu NAJUTA KUZALIWA MWANAMKE

No comments