BABA KIFO NI HAKI YAKO
BABA KIFO HAKI YAKO (1)
IMETUNGWA:JOSHUA
0742873299 SMS/CALL/ WHATSAPP TEXT
Ilikuwa ni ndoa ya namna yake jiji zima lilikodoa macho kutazama ni kitu gani kinaendelea ,barabara nzima zilitapakaa sauti za watu ,pamoja na tarumbeta ,hakika ilikuwa inavutia sana ,Ndugu jamaa na marafiki walimpongeza sana Primi kwa kuoa mwanamke mzuri ,mke wa Primi alikuwa na kila uzuri sio tu umbile na sura hadi tabia yake ilikuwa ni nzuri na yenye kuvutia sana
Baada ya harusi kila mtu alimpongeza primi na kumwambia ``Mkuu hongera sana kama ni mke kweli umepata ‘’
Primi ni meneja wa kampuni kubwa ya vifaa vya ujenzi ijulikanayo kama Arusha civil eginering materials ,kutokana na kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa primi aliweza kupandishwa cheo na kufanywa meneja kwani hapo mwanzo alikuwa katika ngazi ya kawaida kabisa,mkuu wa kampuni alimteua Primi na kumshauri sana ni vyema kuoa ili uweze kufanya kazi kwa ufanisi ,Primi hakusita kabisa alimwoa Recho binti wa mzee Msumi na maisha yaliendelea
Baada ya harusi Primi alimpenda sana mke wake alimfanya kama malaika ,alimpa kila alichokuwa akihitaji alimzungusha kila mahali ,hakika Recho alifurahia sana na kujiona kama malaika ,hakuna alichokuwa akikitaka akakosa ,Bwana wake alimpatia hela za kutosha na ahadi kedekede ,Recho aliishi kama malaika ,ndani ya gari eliza alikaa pembeni ya bwana wake ,hakika walienjoy sana maisha ,waliishi kama malkia na mfalme ,,Baada ya miezi michache kupita Recho alibeba ujauzito ,wakiwa wameketi sebuleni na mume wake ,Recho kwa furaha alimwambia bwana wake
``Baba nikwambie kitu’’
``Usijali mke wangu nieleze nipo kwa ajili yako’’
``Mhhh ,mume wangu upo tayari kusikia hata kama ni mbaya’’ Recho alikuwa akitania
``Ndio usijali kipenzi wewe ndio wangu wa shida na raha ‘’
``Mume wangu jana nilivyoenda kupima nina mimba mume wangu’’
Primi alimrukia mke wake kwa furaha ,alirukaruka juu kwa furaha sana alimshika tena mkewe na kumkumbatia kwa nguvu ,hakika ilikuwa ni raha isiyoelezeka ,kila mmoja alikuwa na raha .kwani ujauzito ni jambo la Baraka sana watu hukesha usiku na mchana wakitafuta mtoto ,hivyo kubeba mimba ni jambo la furaha sana ,
Maisha yaliendelea recho alitunzwa vyema sana na mume wake ,siku zilikata wakati ulitembea hatimaye Recho alijifungua mtoto wa kike ,Primi alifurahi sana ,mtoto wao walimpa jina la Grace ,,,wote kwa pamoja waliishi maisha ya upendo kwa kipindio hicho
BAADA YA MIAKA MITATU
Recho mke wa Primi hakuamini kabisa bado alijiona kama yupo ndotoni ,Primi mume wake aliyekuwa anampenda hapo nyuma leo anamtamkia maneno ya nguoni tena mbele za shoga zake ,Primi anafikia hatua ya kubadili wanawake apendavyo ama kweli hii ilimuuma sana Recho alianza kuamini maneno ya mama yake siku akiwa anamtakia Baraka
``Mwanangu kuwa makini na wanaume leo wanakupenda kesho watakuchoka ,watakudhalilisha ili uweze kuishi nao ,nyenyekea sana kila siku jitahidi kuwa chini zaidi’’
Recho kila akikumbuka maneno ya mama yake alikuwa anapata moyo wa kuendelea kuvumilia vioja vya mumewe ,mume wake aliyekuwa mpole na mtaratibu leo ame mchoka na kumuona kama mavi
Siku moja Recho akiwa ameketi nje ,alisikia sauti ya mtu akibisha hodi ,,Recho alikimbia na kwenda kumfungulia mgeni ,Recho hakuamini macho yake alikuwa ni mama yake mdogo ambaye wana muda mrefu sana hawajaona
Recho alimkumbatia mama yake kwa furaha sana ,kisha walichukuana na kumpeleka sebuleni
Wakiwa wamekaa Primi alikuwa amerejea kutoka kazini ,primi siku hiyo alikuwa na hasira sana ,alipofika nje tu ya nyumba alianza kuropoka
``We mwanamke nakwambia kama umechoka kukaa hapa uondoke ,kwanza hebu muangalie umenenepeana kama nguruwe ,maziwa yamekushuka kama unanyonyesha mayatima ,nakwambia uondoke hapa kama umechoka kuishi hapa ‘’
Mama mdogo wa Recho aliziba masikio hakuamini kama Primi anaweza kumtamkia mkewe maneno kama haya ,Recho alimwambia mama yake
``Mama ndio mateso nayo pata kila siku wala usishangae ‘’
Primi alivyoingia ndani hakuamini macho yake angejua angetulia tu kwani hakujua kama Recho siku hiyo yupo na mama mdogo wake ,Primi alikuwa akiheshimiana sana na mama mdogo wake hivyo alivyoingia ndani tu nakumuona aligeuz spidi ,aliwasha gari na kuondoka ,hakujua atamwambia nini kwa maneno aliyomtamkia mwanae
Ndani ya muda mchache mama mdogo aliondoka na kumwaga grace pia alifurahishwa na mtoto wao Grace kwa sasa alikuwa chekechea na alikuwa na miaka mnne
Siku ziliendelea kusonga Primi aliendelea kufanya vitu vya kumuhuzunisha sana mke wake kwa mara nyingine tena ,primi alitamka maneno mabaya mbele ya rafiki za recho
``Mwanamke gani una shepu kama nguruwe ,tumbo zimefuka ,maziwa yameshuka khaaaaa ukitaka ondoka nakwambia ‘’
Upande wa Primi hakutambua kuwa mwanamke akishajifungua ni ngumu sana mwili wake kuwa kama awali ,Recho alijaliwa umbile zuri sana lililopangilika ila baada tu ya kujifungua alifutuka na kuwa kitu cha tofauti alikuwa mnene sana ,mwili wake wenye uzuri ulibadilika na ndio kawaida kwa wanawake wengi kuwa namna hii
Primi hakulielewa hili alimdhalilisha sana mkewe ilifika wakati hadi mtoto wao mdogo alimfuata baba na kumshika huku akimwambia ``Baba wewe wamgombeza mama ,mama analia sana baba msamehe mama ‘’ Grace alifika hatua ya kuona unyama ambao baba yake anamfanyia mama yake
Siku moja jioni ,Recho akiwa nyumbani anapika ,Grace nae alikuwa pembeni ya mama yake akijifunza kuchora ,wakiwa wametulia walisikia gari la baba likija ,Grace kwa furaha alijisemea
``Baba huyooooo baba huyooo kaleta zawadiii ‘’
Ndani ya dakika mbili Primi alifunguliwa geti na mkewe ,Recho hakuamini macho yake ,ndani ya gari akishuka mwanadada mrembo sana aliyejipodoa akapodoka ,sura na shepu yake vilikuwa siyo vya nchi hii ,kikubwa sana kilichomfanya Recho kushindwa kuvumilia ni pale
Primi mume wake wa ndoa alipomshika dada Yule na kumkiss kisha akapigana nae denda hadharani kabisa
Recho uvumilivu ulimshinda alimrukia primi kwa nguvu na kumwambia ``Primi mume wangu unadiriki kunifanyia hivi mbele ya mwanao ,unanisaliti mbele ya macho yangu ,Primi ,Primi Mungu yupo nasema Mungu yupo ‘’
Kwa hasira Primi alimpiga mkewe kofi moja zito hadi mke wake aliweweseka na kudondoka chini ,grace alipomwona mama yake amepigwa alianza kulia kwa uchungu huku akisema
``Baba ,nakuomba baba usimpige mama ,usimpige mama baba ‘’ grace alilia sana na udogo wake wote hakutamani kumwona mama yake akilia
Recho akiwa chini ,Primi mume wake alimkanyaga tumboni kama mtu anashindilia gunia huku akimshushia matusi ``Mpuzi wewe nakwambia kuanzia sasa wewe na mdoli wako muondoke ,wewe kwanza siyo type yangu mnitoke muone tumbo kama kiroba cha mchele ondoka ‘’
Msichana Yule alimvuta primi na kumwambia ``baby twende ndani bhana achana na huyu tipwa tipwa ‘’
Recho akiwa chini alisikia maneno ya mwanamke yule ,yalipenya sawia masikioni
Je nini kitaendelea ………………………………………………………………………………………………..
Simulizi hii inapatikana yote kwa sh 1000 usiache kununua kwani utajifunza mengi sana kuhusu ndoa na maisha kwa ujumla ,lipa sh 1000 kwa namba 0742873299 jina Martha ukishalipa nitumie msg au njoo fb inbox au whatsapp nikurushie 0742873299 whatsapp
BABA KIFO NI HAKI YAKO (2)
0742873299 WHATSAPP
Recho uvumilivu ulimshinda alimrukia primi kwa nguvu na kumwambia ``Primi mume wangu unadiriki kunifanyia hivi mbele ya mwanao ,unanisaliti mbele ya macho yangu ,Primi ,Primi Mungu yupo nasema Mungu yupo ‘’
Kwa hasira Primi alimpiga mkewe kofi moja zito hadi mke wake aliweweseka na kudondoka chini ,grace alipomwona mama yake amepigwa alianza kulia kwa uchungu huku akisema
``Baba ,nakuomba baba usimpige mama ,usimpige mama baba ‘’ grace alilia sana na udogo wake wote hakutamani kumwona mama yake akilia
Recho akiwa chini ,Primi mume wake alimkanyaga tumboni kama mtu anashindilia gunia huku akimshushia matusi ``Mpuzi wewe nakwambia kuanzia sasa wewe na mdoli wako muondoke ,wewe kwanza siyo type yangu mnitoke muone tumbo kama kiroba cha mchele ondoka ‘’
Msichana Yule alimvuta primi na kumwambia ``baby twende ndani bhana achana na huyu tipwa tipwa ‘’
Recho akiwa chini alisikia maneno ya mwanamke yule ,yalipenya sawia masikioni
Recho alitamani anyanyuke afanye vurugu ila aliona haita saidia kitu ,alishuhudia kwa macho yake mumewe akiongozana na Yule mwanamke kuingia ndani hakika hii ilimuuma sana sana
Grace alimfuata mama yake ,alipomwona mama yake mzazi analia na yeye alijikuta akishikwa na uchungu alilia sana
Ndani Primi alichukuana na binti yule wakaingia bafu za ndani bila hata stree waliogeshana huku wakipeana mahaba baada ya hapo waliekea ndani alifanya uchafu wao kwa zaidi ya masaa matano ilipofika saa tatu za usiku primi alichukuana na mwanadada Yule kisha aliwasha gari na kumrudisha kwake ,hakika Recho aliumwa roho kwani alisalitiwa mchana kweupe
Mume wake siku hiyo hata nyumbani hakurudi ,grace na mama yake walibaki nyumbani wenyewe ,ilipofika usiku grace alimuuliza mama ``Mama baba yuko wapi ,alafu mama mbona baba anakupiga sana mimi sipendi’’
``Mwanangu lala mwaya usijali ,lala baba yako ni mzuri hana tatizo lala na anakupenda ‘’
Recho hakutaka kumpandikizia mwanae roho mbaya ya kumchukia baba hivyo alijitahidi sana kumridhisha kwa kumwonyesha kuwa baba yake ni mzuri ila kumridhisha huko hakukuingia akilini mwa grace kwani grace alijua wazi mama yake ana teseka sana
BAADA YA SIKU MBILI
Zilipopita siku mbili Primi alikuja tena na mwanamke Yule pale nyumbani ,kwa hasira recho alijisemea ``Leo liwalo na liwe lazima nimtoe alama huyu mwanamke kwanini ana niibia mume wangu wakati mimi nipo hai ,hakika sikubaliani na hili ‘’
Recho aliingi jikoni alitoka na kikombe cha chuma chenye mafuta ya moto kabisa ,recho alikuwa akirosti ndizi zake hivyo mafuta bado yalikuwa yapo jikoni ,alipofika nje na kikombe chake ,primi nae alikuwa akiingia huku akiwa amemshikilia mrembo ,alipofika karibu na mke wake primi alisema
``Toka mbele yangu kabla sijatapika muone kwanza na mitumbo yake iliyojaa upepo ,mwanamke shepu mbovu’’ mrembo Yule alicheka kwa nguvu huku akisema
``hahahahaahah haloooooooooooooooo wewe mwanamke si uondoke unakuwa king’ang’anizi kama kupe huyu hakupendi ,hupendwi unajishikashika tu kama ni mtoto mwache tutamtunza wewe ondoka shenziiiiii’’
Recho alikuwa tu akimsubiri mwanadada Yule aropoke ,alipomaliza kuongea ,recho alimwagia mwanamke Yule mafuta ya kupika ya moto usoni ,,Heeeee dada Yule alipiga kelele kubwa kwa maumivu
``Nakufaaaa eeee Mungu wangu nisaidieee Primi nionee huruma uzuri wangu umetoweka ‘’
Dada Yule ngozi ilitoka alichubuka vibaya alitokewa na majipu makubwa yaliyovimbia maji ,alilia hadi akajikojolea ,hakika hakuna kitu kinauma kama kuchomwa na mafuta ya moto ,unaweza kutamani dunia ipasuke
Kwa hasira Primi aliingia ndani alikuja na rungu ya chuma alimkamata mkewe alimlaza chini
Alihakikisha ameuvunjavunja mkono wake ,hadi mfupa ulionekana ,grace mtoto mdogo alishuhudia mama yake akifanyiwa ukatili wa ajabu kwa woga huku akilia sana alisema
``Baba msamehe mama ,baba usimuue mama bado nampenda mama yangu ‘’ grace alilia huku akimaanisha sana ,kilio kilitoka ndani kabisa ya moyo
Recho alipiga kelele kubwa ila ndio tayari mkono ulikuwa umeshavunjwa na Primi ,grace alimkamata baba yake suruali na kumwambia
``Baba mwache mama anatoa damu utamuua ‘’
Kwa hasira Primi alimpiga teke la nguvu grace ,maskini mtoto mdogo alidondokea ng’ambo ya pili
Yaan vilio vilitapakaa hapo nyumbani ,primi alipomtazama mrembo wake alikuwa hatamaniki kwa haraka alichukua gari na kumwaaisha kahaba Yule hali amemvunja mkewe mkono damu zinamtoka mkewe mithili ya chemichemi
Itaendelea …………………………………..
Jipatie simulizi nzima kwa sh 1000 usipitwe na mkasa huu wa kusisimua fanya malipo kwa namba ya mpesa 0742873299 jina martha ukisha fanya malipo njoo sasa inbox whatsapp upatiwe simulizi nzima njoo whatsapp 0742873299 whatsapp/sms/call
itaendelea yote ndani ya blog yetu ,ila waweza ipata simulizi nzima kwa sh 1000 tu

No comments