NAJUTA KUZALIWA MWANAMKE 17


Najuta kuzaliwa mwanamke 17

Jesca alipoamka alielekea moja kwa moja sebuleni ,alipofika alimkuta mama mkwe akiwa pamoja na baba na cathe ,kabla jesca hajamalizia salamu mama mkwe alipayuka
``wewe ndio boss ee ,unalala hadi sasa hivi siyo ‘’’
Jesca alinyamaza kimya hakujibu  kitu kwani alikua amekosea cha zaidi alisema
``nisamehe mama ‘’
``mshenzi wewe ,lazima nikunyooshe kwanza ‘’
Mama mkwe aliamka na kumfuata jesca ,akiwa anaenda baba mkwe wa jesca alimvuta mkewe mkono
``mke wangu umesahau jana usiku kilichotokea ‘’
``Ya jana usiku ni jana usiku lazima nimnyooshe huyu zumbukuku hajui maisha huyu’
Jesca akiwa amesimama alimwona mama mkwe akimsogelea kwa haraka ,mama mkwe alimzibua jesca kibao cha nguvu ``paaaaaaaaaaaa!!!!’’
Jesca alinyamaza kimya ,akiwa ametulia kibao kingine kilipigwa tena paaaaah!!!!!!!!!!!!!!!!!
Mama mkwe alisahau yaliyomkuta jana ,ila kabla hajarudi kwenye sofa alisikia sauti kubwa iliyoijaza nyumba
``mama angu sina jinsi ya kukusaidia nilikusamehe ila naona sasa umeamua kufanya yale yale ufanyayo  ,lazima nikuue ‘’
Mama mkwe alianza kupiga kelele
``nisamehe mwanangu usiniue Hussein usiniue ‘’
Kila mtu aliyekuwa pale alimshangaa mama mkwe kwani mama mkwe alikua kama mtu aliyechanaganyikiwa ,,ndani ya dakika mbili mama mkwe akili zilifyatuka alianza kuvua nguo zake
Alibaki mtupu kabisa ,,,mume wake akishirikiana na cathe walifunga milango asiweze toka
Ila mama mkwe alikua na nguvu kupindukia ,aliwasukumia mbali na kutoka nje akiwa uchi wa mnyama huku akisema
``Hussein mwanangu usiniue ,nisamehe mwanangu,nisamehe eee’’
Cathe alikimbizana na mama yake kwani alijua mama yake kuwa hivyo ni aibu sana
Baba mkwe alimfuata jesca na kumbembeleza huku akisema
``mwanangu katika hili haupo mwenyewe naona maonevu yamezidi hadi Mungu kaingilia kati naamini manyanyaso yote yanamwisho jipe moyo mkuu ,mali zote hapa ni zako ondoa shaka ‘’
``asante baba kwa kunifariji ‘’ jesca alimshukuru baba mkwe
Wakiwa wanaendelea kuongea taarifa ziliwajia
``Baba Cathe mkeo hali yake ni mbaya ameshikiliwa huko nje ,jitahidi ukamsaidie ‘’
Mama mkwe alishikwa na uchizi kabisa watu walikimbia nae huku na huko ili waweze kumkamata kwani alifanya vimbwanga vya ajabu
Baba mkwe alitoka nje kuambatana na umati wa watu waliokuwa wakimtazama chizi wa kike ‘’
Jesca akiwa sebuleni alisikia sauti ya mumewe
``yaliyo na mwanzo yana mwisho ishi ukimtegemea Mungu ,tunza mimba yangu naamini muda siyo mwingi utaniletea mwanangu duniani ,ataitwa happy yaan furaha ya ulimwengu’’
Itaendeleaa………………………..
Jesca alifarijika sana ndani ya moyo wake alijua yote yatawezekana na ndani ya muda mfupi amani itatawala ,kitu kilichompa matumaini sana jesca ni kuwa kila aliyesimama mbele yake kama kikwazo ,hakuchukua muda mrefu alipatwa na janga kubwa sana ,,jesca alijenga imani yake kwa Mungu na aliamini kabisa dunia hakuna baya mtu analofanyiwa lisilipwe ,hata kama siyo leo ni kesho ,kama siyo kesho ni kesho kutwa
Baada ya makimbizano marefu ,waliweza kumkamata mama mkwe na kumfunga kamba kwani alikua akifanya mambo mabaya ya ajabu
Mama mkwe aliletwa akiwa amefungwa kamba mikononi na miguuni ,muda wote mama mkwe alikua akipiga kelele ``mwanangu usiniue ,usiniue jamaniii eee nisamehe mara ya mwisho mwanangu’’
Jesca alimsogelea mama mkwe wake na kuushika mkono wake kisha alimwambia
``nimekusamehe mama yangu’’
Jesca alipomaliza kusema tu hayo fahamu zilimrudi mama  mkwe ,,,kila mtu alishangaa
Watu walianza kuzngumza chinichini
``daah kweli Mungu wa ajabu kumbe hii ni laana tu ya huyu binti ,sema kweli ata akiwa chizi awe tu maana alimtesa sana huyu binti yaan unamfukuza mtu ambaye amebeba mimba ya mwanao’’
Mama mkwe alipata nafuu kabisa akili zake uelewa wake ulirudi asilimia zote ,alikua mzima kabisa
BAADA YA MIEZI TANO
Mimba ya jesca ilikua kubwa na tayari alikuwa ametimiza miezi tisa ,jesca alipendwa sana si baba mkwe ,mama na wifi  wote walimpenda ,waliishi kwa amani sana ,wote waliamini kabisa mimba aliyo nayo jesca ni ya husein marehemu ,hivyo walimtunza vyema kwani walikuwa wakisaidia damu yao
Siku zilipoenda jesca alijisikia hali ya tofauti alijua hapa siku si nyingi atajifungua
Taratibu jesca alichukuana na wifi ake na kuelekea hospitalini ,jesca akiwa na mimba yake kubwa alipelekwa wodi namba 10 ,huko alikutana na wamama wajawazito wengine ambao siku si nyingi watajifungua
Jesca akiwa katika kitanda chake ametulia ,nesi mmoja alimfuata na kumwambia
``sema ni tarehe gani utajifungua ‘’
``nesi sijui nadhani ni mwezi huu ndio wa tisa’’
Nesi Yule alicheka kwa dharau
``muonee aibu  yako kazi ni kupandana pandana  tu kama mbwa hujui hata tarehe utakayojifungua ,aibu yako au mimba ya kubakwa hii’’
Maneno ya nesi yalimchoma sana jesca ,jesca alitamani ampige nesi Yule ,ki umri nesi Yule alikua ni mdogo kabisa hata kwa mwonekano alionyesha ,ila dharau alizokuwa nazo siyo za nchi hii
Nesi Yule alimfuata jesca na kuanza kuminyaminya tumbo la jesca kama mtu anayeminya parachichi ambalo bado halijaiva vyema
Akiwa anaminya alimsemesha jesca
``we mwanamke wewe kitumbo chako ka pulizo lililotoka upepo ,hii mimba wenda haijafikia wewe ‘’
Jesca kwa hasira alishindwa kuvumilia kero za nesi
Alichukua mercury (kemikali kali sana) iliyokuwa pembeni  alimrushia nesi Yule na kumwagikia mikononi,mercury ni hatari sana ,ilianza kumchoma nesi Yule ,nesi Yule aliita kwa nguvu kuwashtua wenzake wamsaidie
Nesi na daktari wa zamu walifika na kumsidia mwenzao
``hey dada secy nini shida jamani mercury si tulisema ikae maabara mbona mmeileta humu’’
secy  alijibu kwa nguvu
``ni huyo ndio kanimwagia plz ‘’
Nesi mmoja anaitwa Katarina alimfuata jesca na kumwambia
``makubwa madogo yananafuu sasa wewe mama utajibeba ,unamumiza nesi ambaye atakuzalisha wewe unategemea nini’’
Huwezi amini wakati ule ule uchungu ulimfika jesca ,jesca alianza kupiga kelele za kuhitaji msaada wa kujifungua ‘’
Manesi wote walikimbia na kusema
``huyu mwananamke mshenzi anamwagia mwenzetu mercury’’
Laiti kama wangejua kuwa  nesi secy ndiye wa kwanza kuongea kashfa kwa jesca
Jesca akiwa kitandani alipiga kelele za uchungu ,huwezi amini dakika tano zilipita kimya
Upande wa pili mama mkwe wa jesca alikuja na gari lake kwa haraka sana hospitalini pale alipofika alilipaki nje kisha alizama wodini
Alipofika kitandani mwa jesca alikuta tayari damu zinamvuja jesca mtoto ndio huyo anakaribia kutoka ,mama mkwe alipotazama pembeni hakuona muuguzi hata mmoja alikimbia hadi ofisi kuu
Alipofika kila muuguzi alitetemeka sana walimwogopa mama mkwe kwani mwonekano wake tu uliktosha kuwashughulisha
Ndani ya dakika moja walielekea ,mama mkwe alibaki mwenyewe huku akisema
``hahahahaha mimi naogopeka hivi utadhani mimi ni waziri ‘’
Akiwa anawaza vile wazo chafu lilimjia mama mkwe alijisemea
``hivi manesi nikiwapa kitu kidogo waue hiki kichanga si dakika mbili tu ,waulie mbali kwanza huyu  mtoto haijulikani hata baba ni nani’’
Akiwa anawaza hayo nesi secy alipita
``samahani dada ‘’
`bila samahani’’
``ok nitakupa chochote utakacho waweza kukiua kichanga cha huyu binti ‘’
`kwanini mama kuna tatizo ‘’
``ndio mtoto anaugomvi wa kifamilia ‘’
``ok mama njoo pembeni’’
Secy alimnong’onezea mama mkwe
``shilingi laki tatu ‘’
Mama mkwe alipiga mkono kwenye begi kisha alitoa nusu ya hela ile  yaan laki moja na nusu
Kisha alimpa nesi secy ,secy alifurahi alimwambia
``si mtoto tu afe au niue na mama ake ‘’
``ungeweza hata wote ni sawa mwanangu’’
Nesi secy alirudi wodini kwa haraka
``je nini kitaendelea ………………………………………

No comments

Theme images by jangeltun. Powered by Blogger.