NAJUTA KUZALIWA MWANAMKE 16
NAJUTA KUZALIWA MWANAMKE 16
Upande wa pili jesca akiwa usingizini ndoto nzuri ilimvaa
Aliota yupo chini ya mti wa kivuli ,,,,akiwa amekipakata kichanga chake ,pembeni yake alikuwepo Hussein mume wake ,,akiwa anazishikashika nywele za katoto huku akisema
`mwanangu nakupenda wewe ndio faraja yetu ,,,’’
Hussein alimchukua mtoto akampakata kisha akambusu mtoto pamoja na jesca
Jesca alipopigwa tu busu tu ghafla na yeye alizinduka usingizini
Jesca alitamani hadi kulia alipojitazama aliona machozi yakiwa yamejaa mashavuni akiwa anafikiria juu ya ndoto ile alisikia sauti ya mama mkwe
``Hussein usiniue usiniue mwanangu’’
Mama mkwe alikua akipiga kelele kama mwehu
Mama mkwe alikua kama mtu aliyechanganyikiwa aliendelea kupiga kelele tu kama kichaa
Jesca nae alienda kutazama kuna nini ,alipofika Chumbani kwa mama mkwe na baba mkwe ,alimkuta mama mkwe akipiga kelele kama mwehu ,Mama mkwe alipomwona jesca alinyanyuka na kumfuata kisha alipiga magoti chini yake na kusema
``mwanangu naomba unisamehe nisamehe kwa yote niliyokutenda ,nisamehe ,nisamehe ‘’
Jesca alitokwa na machozi hakuamini kabisa kama mama mkwe wake anaweza kumwomba msamaha
Jesca alimjibu mama mkwe
``Sawa mama nimekuelewa nimekusamehe ‘’
Mama mkwe alifurahi alisimama na kukumbatiana na jesca
Kwa sababu ilikua bado usiku wa manane ,kila mmoja alirudi kwenye chumba chake kuendelea kupumzika ,jesca aliorudi ndani ,cathe nae alirudi ndani ,baba mkwe alimshika mke wake na kumwambia
``usijali mke wangu ni ndoto tu wala Hussein hawezi kukuua ,ondoa shaka kabisa ‘’
``Sawa kipenzi change tulale baba ‘’
Baba cathe hakuamini kama mkewe anaweza kuwa mpole namna hiyo
Wote kwa pamoja walilala na kupumzika
Ilipofika asubuhi ,mama mkwe alimka asubuhi na kuandaa chai kwa ajili ya familia yake
Kutokana na uchovu ,Jesca alilala sana alishtuka amezinduka saa tatu za asubuhi
Jesca alipoamka alielekea moja kwa moja sebuleni ,alipofika alimkuta mama mkwe akiwa pamoja na baba na cathe ,kabla jesca hajamalizia salamu mama mkwe alipayuka
``wewe ndio boss ee ,unalala hadi sasa hivi siyo ‘’’
Jesca alinyamaza kimya hakujibu kitu kwani alikua amekosea cha zaidi alisema
``nisamehe mama ‘’
``mshenzi wewe ,lazima nikunyooshe kwanza ‘’
Mama mkwe aliamka na kumfuata jesca ,akiwa anaenda baba mkwe wa jesca alimvuta mkewe mkono
``mke wangu umesahau jana usiku kilichotokea ‘’
``Ya jana usiku ni jana usiku lazima nimnyooshe huyu zumbukuku hajui maisha huyu’
Jesca akiwa amesimama alimwona mama mkwe akimsogelea kwa haraka ,mama mkwe alimzibua jesca kibao cha nguvu ``paaaaaaaaaaaa!!!!’’
Jesca alinyamaza kimya ,akiwa ametulia kibao kingine kilipigwa tena paaaaah!!!!!!!!!!!!!!!!!
Mama mkwe alisahau yaliyomkuta jana ,ila kabla hajarudi kwenye sofa alisikia sauti kubwa iliyoijaza nyumba
``mama angu sina jinsi ya kukusaidia nilikusamehe ila naona sasa umeamua kufanya yale yale ufanyayo ,lazima nikuue ‘’
Mama mkwe alianza kupiga kelele
``nisamehe mwanangu usiniue Hussein usiniue ‘’
Kila mtu aliyekuwa pale alimshangaa mama mkwe kwani mama mkwe alikua kama mtu aliyechanaganyikiwa ,,ndani ya dakika mbili mama mkwe akili zilifyatuka alianza kuvua nguo zake
Alibaki mtupu kabisa ,,,mume wake akishirikiana na cathe walifunga milango asiweze toka
Ila mama mkwe alikua na nguvu kupindukia ,aliwasukumia mbali na kutoka nje akiwa uchi wa mnyama huku akisema
``Hussein mwanangu usiniue ,nisamehe mwanangu,nisamehe eee’’
Cathe alikimbizana na mama yake kwani alijua mama yake kuwa hivyo ni aibu sana
Baba mkwe alimfuata jesca na kumbembeleza huku akisema
``mwanangu katika hili haupo mwenyewe naona maonevu yamezidi hadi Mungu kaingilia kati naamini manyanyaso yote yanamwisho jipe moyo mkuu ,mali zote hapa ni zako ondoa shaka ‘’
``asante baba kwa kunifariji ‘’ jesca alimshukuru baba mkwe
Wakiwa wanaendelea kuongea taarifa ziliwajia
``Baba Cathe mkeo hali yake ni mbaya ameshikiliwa huko nje ,jitahidi ukamsaidie ‘’
Mama mkwe alishikwa na uchizi kabisa watu walikimbia nae huku na huko ili waweze kumkamata kwani alifanya vimbwanga vya ajabu
Baba mkwe alitoka nje kuambatana na umati wa watu waliokuwa wakimtazama chizi wa kike ‘’
Jesca akiwa sebuleni alisikia sauti ya mumewe
``yaliyo na mwanzo yana mwisho ishi ukimtegemea Mungu ,tunza mimba yangu naamini muda siyo mwingi utaniletea mwanangu duniani ,ataitwa happy yaan furaha ya ulimwengu’’
Itaendeleaa………………………..
No comments