NAJUTA KUZALIWA MWANAMKE 04
NAJUTA KUZALIWA MWANAMKE 4
mahali salama
Upande wa pili salum au baba kenedy aliwaza sana juu ya mtoto jesca ,alijaribu kulala ila usingizi ulimruka kabisa hakuwa na hata lepe la usingizi ,alipomtazama mkewe alimwona mkewe amechapa usingizi ,taratibu aliamka huku akinyata alitoka na kuelekea chumba cha wageni aliko jesca
Jesca akiwa amelala alisikia mlango wake ukiguswa ,jesca alishtuka sana kwani hakujua ni nini
Jesca alipotazama alimwona salum akiwa mbele yake akiwa amevalia bukta na sing’lendi nyeupe
``samahani sana najua umeogopeshwa na mimi kuwa hapa ,mapenzi yameujaza moyo wangu nimeshindwa kulala bila kukuona wewe naomba unipe nafasi ya kuwa nawe hata kwa nusu saa nitakulinda na kukufikisha kwenu salama ‘’
Jesca alitetemeka hakuwahi kuamini kama kitu kama kile kitamtokea ,kwa haraka alikumbuka maneno ya mama kenedy mke wa salum `` nakuomba uwe makini mume wangu si mwaminifu sana hivyo ukiona analeta mazoea ya ajabu muepuke au uniambie’’
Jesca alijikuta akishikwa na kigugumizi akisema ``sii-weziii-nisamehe-bure’’
Salum alisogea hadi kitandani na kuketi karibu nae
Upande wa pili mama kenedy alizinduka usingizini ,alipotazama pembeni hakumwona mume wake ,kwa haraka alikurupuka na kutoka ndani alijua hapa kuna kitu kinaendelea siyo kawaida
SONGA NAMI………………………………………………………………………………………………………………………………
Salum alimshika jesca mkono huku akisema
``jesca unataka niseme nini ili ujue nakupenda nipe hata dakika tano za kuwa nawewe kipenzi ‘’
``hapanaa haiwezekani ‘’
Salum aliendelea kunang’ania ,akiwa amemshika jesca mkono ,mama kenedy alizama chumbani kwa haraka kisha alisimama wima akiwatazama jesca na baba kenedy
Jesca alianza kujitetea
``mama amekuja mwenyewe nimemkatalia ananilazimisha mama angu’’
Baba kenedy alimtazama jesca kwa jicho la ukali sana ,jesca alipoona jicho hilo alinywea kama uji wa mhogo alijikuta akishikwa na aibu ,mama kenedy kwa jazba alianza kutukana
``wewe kahaba uliyekubuhu tumekuleta hapa tukidhani unakuja kutusaidia hatimaye unatuletea uhuni na ufuska unataka kulala na bwana angu ‘’
``hapana mama hapana ni yeye amekuja’’
``nyamaza mjinga wewe umekuja na vimtego vyako sikia wewe kahaba huyu ni mume wangu kama unataka kuishi hapa mweshimu sawa ‘’
Jesca alijibu ``sawa mama naomba unisamehe ‘’ jesca alitubu hadi makosa ambayo hajakosea yeye ,hakika jesca alipatwa na wakati mgumu
Mama kenedy alimshika mume wake mkono na kurudi nae ndani,huku wakiongea
``hivi baba kenedy umekosa nini kwangu ,kitu gani umekihitaji ukakosa au ni huyu binti kakuzuzua ‘’
``mke wangu ee naomba tukalale haya achana nayo ‘’
Baba kenedy alikua ni mkali sana ,mara nyingi amekua akimpelekesha sana mkewe kwani ,
mkewe hana kazi yoyote ya kufanya anamtegemea baba kenedy katika kila jambo ,hii imemfanya mama kenedy kukosa sauti juu ya mume wake ,mara nyingi sana katika familia yao wameshindwa kuishi na mabinti wa ndani kwani baba kenedy amekua akiwarubuni kimapenzi jambo ambalo lilikua likimumiza sana mama kenedy
jesca alirukwa na usingizi usiku kucha ,hakupata hata lepe la usingizi ,alikua akiwaza sana yaliyotokea ,sauti ya mama kenedy akigomba iligonga ndani ya akili ya jesca
``wewe kahaba uliyekubuhu tumekuleta hapa tukidhani unakuja kutusaidia hatimaye unatuletea uhuni na ufuska unataka kulala na bwana angu ‘’
Jesca aliwaza ni lipi baya amefanya ila hakupata jibu alijisemea
``kesho majaliwa lazima niombe kuondoka maana hapa sipawezi kabisa ,ila nitaenda wapi mimi maana sijui hata niko wapi ‘’
Ilipofika asubuhi jesca aliamka na kusaidiana na mama kenedy kuaandaa chain a vitafuno ,baada ya kuandaa ,baba kenedy alikunywa na kuwaaga
``jamani wacha mimi niende kazini tutaonana baadae ‘’
Mama kenedy alimkimbilia mume wake na kumkunja kola za shati yake kisha alimkiss
``mwaaaaaa kazi ,kazi njema baba usisahau kuniletea ile zawadi sawa kipenzi ‘’
``usijali mke wangu ‘’
Baba kenedy aliwasha gari kuelekea kazini ,alimwacha jesca na mama kenedy nyumbani pale
Baba kenedy alivyokuwa akitoka getini mlinzi wa geti alimfungulia huku akimwambia
``mzee baba vipi ,boss hongeraa jana naona umeingia na sukari yao ,mtoto mzuri Yule mfanyakazi nini boss au mke wa pili tujue ‘’
``mrema wacha maneno yako wewe ‘’
``mhhh boss najua wewe ni mzee wa totos hapo wenda ushamaliza mambo’’
Baba kenedy hakupendezwa na utani wa mlinzi wake alimwambia kwa ukali
``naona tunavunjiana mipaka sasa fanya kilichokuleta hapa sawa ‘’
Huku akichekacheka mrema aliitikia
``sawa boss samahani sana ‘’
Baba kenedy aliondoka na gari yake kuelekea kazini
Mama kenedy alibaki na jesca nyumbani ,,,baada ya shughuli za asubuhi alimwita jesca
``weee jesca hebu njoo,upo ndani unafanya nini sasa hizi ,huoni ndani hakujadekiwa ,cha mchana hakijapikwa hujaogesha mwanangu ,sikia mama hapa haujaja kushangaa magari piga kazi sawa ‘’
``sawa mama kenedy nimekuelewa ‘’
Jesca alijibu huku akifuatilia dekio kwa ajili ya kusafisha nyumba
Baada ya jesca kumaliza kila kitu mama kenedy alimwita tena na kumwambia
``sasa sikia shoga angu ,sijui mwanangu ,sijui mdogo angu wewe ,yote sawa tu nikikuita moja wapo ‘’
Mama kenedy alifunga kanga yake kiunoni na kumwambia jesca
``ukitaka kuona hapa ni pachungu ole wako nikuone na baba kenedy kipenzi changu ,nakwambia siyo tu nikuone hata nikuhisi una mahusiano nae utashaa ,nitakua nakuapia sawa wewe ‘’
``mhhh sikia mama kenedy jana alinifuata ndani mwenyewe mimi nifanyaje ,nilimkatalia ndio maana ukamkuta ameketi pale ‘’
``sitaki kusikia maneno yako sijui kimeshuka kimepanda nasema nisikae nikuone umesimama na mume wangu mipaka iwepo sawa’’
Jesca alijikuta akijibu kiunyonge
``sawa mama kenedy ‘’
``ok unaweza kuendelea na majukumu ‘’
Jesca aliondoka huku akisononeka sana moyoni alijisemea
``Mungu wangu nimekukosea nini hapa penyewe nilidhani pana nafuu ila nikibarua tena laity kama ningejua hapa ni wapi na laiti kama ningekua na nauli ningerudi kwetu tu’’
Ilipofika jioni baba kenedy alirudi ,aliporudi familia nzima ilikua na furaha si mama si watoto ,baba kenedy alimletea kila mtu zawadi ,mama kenedy alipewa kanga doti tatu ,watoto waliletewa vigari vya kuchezea na midoli ,baada ya kuwapatia baba kenedy alisema
``jesca yuko wapi nipo na zawadi yake ‘’
Jesca nae alipewa kanga doti moja,jesca alishukuru sana na kuipeleka ndani ,alivyoipeleka ndani tu mama kenedy alimkimbilia nyuma yake na kumfuata ndani ya chumba chake
``sikia wewe nguruwe kitendo cha wewe kupewa kanga isiwe ndio kigezo cha kujifanya mke mwenza ,nitakutoa roho mwanakwenda wewe huna lolote
Jesca alichukia sana kwa hasira alimrudishia mama kenedy
``mama kama vipi chukua tu sitamani hiki kiwe chanzo cha ugomvi sawa ee’’
``mpuzi wewe usijitie una kiburi ,chukua kanga hii maskini wewe ila ole wako umkaribie mume wangu’’
Ilipofika jioni wakiwa dining (sehemu ya kulia ) kwa nje walisikia kelele
Mama kenedy jamani shoga ako kapatwa na majanga njoo msaada tafadhali
Mama wa jirani mama subira aliuguliwa na mtoto wake ,mtoto wake alipatwa na malaria ya ghafla ,mama kenedy kwa haraka aliingia ndani na kujitupia kitenge ili aongozane na shoga ake kwendaa hospitalini
Nyumbani pale alibaki baba kenedy ,watoto pamoja na jesca
Mama kenedy alipoondoka baba kenedy alijisemea
``ama kweli bahati ikija haibishi hodi huu ndio muda niliokuwa nikiutafuta ‘’
Kwa haraka aliwaambia wanae
``kenedy na glory mkapumzike kesho shule sawa wanangu ‘’
Watoto walimwaga baba ``usiku mwema baba anti jesca usiku mwema ‘’
Waliondoka na kuingia katika chumba chao
Baba kenedy alirudisha macho kwa jesca huku akisema
``jesca mama vipi kula mrembo ‘’
``Sawa baba kenedy nakula ‘’
``au nije nikulishe ‘’ baba kenedy alinyanyuka na kwenda kukaa karibu na jesca alimshika jesca mkono na kuanza kumlisha
``baba kenedy naona unachokifanya si sahihi ‘’
``hapana usijali jamani mbona mambo ya kawaida ‘’
Baba kenedy alimshika kwa nguvu jesca aliyekua akifurukuta kujitoa katika mikono yake
Upande wa pili mama kenedy alivyofika kwa shoga ake mama subira alimkuta baba subira akiwa nje
``haaa mama kenedy jamani mwenzako kashatangulia pikipiki imekuja fasta tumemwahisha ‘’
``jamani sawa baba subira nitakuja kesho kuwajulia hali’’
Mama kenedy safari yake iliishia hapo alirudi nyumbani kuendelea na mambo mengine
Baba kenedy alisumbuana sana na jesca ,hatimaye jesca alikua mpole ,baba kenedy alimshika jesca na kuanza kumbusu hali wakiwa sebuleni
Mama kenedy nae alifika nyumbani ,bila hata hodi alijipeleka moja kwa moja hadi sebuleni alichokumbana nacho kilipandisha wazimu wake
``wewe mpuzi nilikwambia usilogwe ukamkaribia bwana wangu hahahah hunijui mimi binti wa kizaramo mtoto wa mzee ngaleshi ;’’
Baba kenedy alijua kichaa cha mke wake kwa haraka alimwachia jesca ambaye alikua amemshikilia alikimbilia nje kuwaacha wapambane
Mama kenedy alikua jeuri sana alimfuata jesca na kumzaba makofi kama mvua ``paaaah paah paaah’’
Mama kenedy alisogea pembeni na kuchukua pasi ya umeme iliyokuwa pembeni aliongeza moto hadi mwisho ,alimkokota jesca hadi ilipo pasi
Jesca alipambana huku akisema ``mama kenedy niamini shida ni huyu bwana wako siyo mimi hata Mungu anaona ‘’
Mama kenedy wazimu wake ukimpanda anakuwa na nguvu kama simba alimzaba jesca kibao kimoja
Jesca alidondoka hadi chini kwenye kapeti
Mama kenedy alichomoa pasi kwenye moto ,alimvua jesca nguo za juu ,bila huruma alipitisha pasi ya moto mgongoni mwa jesca
Jesca alipiga kelele moja kubwa sana iliyoambatana na uchungu wa hali ya juu ,isauti aliyotoa jesca iliwavuta majirani ,mlinzi na wapitia njia kuja kushuhudia nini kinafanyika
Je nini kitaendeleaaa
Share like na comment

No comments