AHUKUMIWA MIAKA 30 JELA KWA KUBAKA MWANAFUNZI
Imeelezwa mbele ya mahakama ya Wilaya ya Chato kuwa mshtakiwa alikamatwa na polisi Oktoba 7, mwaka 2019, na kwamba baada ya mahojiano ya awali alikiri kufanya mapenzi na mtoto huyo (jina tunalo), ambaye ni mwanafunzi wa shule ya msingi Maweni Kata ya Buseresere.
Mwendesha Mashtaka wa serikali, Erasto Anosisye akishirikiana na Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Mauzi Lyawatwa, waliieleza mahakama hiyo mshtakiwa alitenda kosa la kumbaka mtoto aliye chini ya miaka 18 kinyume cha sheria.
Walidai tendo la kufanya ngono na mtoto ni kosa la jinai ambalo linaangukia kwenye kifungu cha sheria namba 130(1) na 2(e) pamoja na kifungu namba 131(1) cha sheria ya makosa ya jinai.
Waliiomba Mahakama iwapo itamkuta na hatia mshtakiwa apewe adhabu kali kutokana na kukithiri kwa vitendo vya ubakaji kwa watoto, ambavyo vimekuwa vikidhoofisha malengo ya serikali ya kumpatia elimu mtoto wa kike, magonjwa ya ngono na hata mimba za umri mdogo.
Baada ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Denice Mrashani, kusikiliza maelezo ya pande zote mbili, alisema mahakama hiyo imejiridhisha pasipo kuacha shaka kuwa mshtakiwa anayo hatia dhidi ya kosa analoshtakiwa nalo, huku akimpatia fursa ya kuiomba mahakama kumpunguzia adhabu.
Katika utetezi wake, Maliatabu ameomba kupunguziwa adhabu kwa kuwa hana ndugu karibu na kwamba amekaa gerezani akiwa mahabusu muda mrefu.
Mahakama hiyo ilimhukumu kifungo cha miaka 30 jela ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye kufanya vitendo hivyo.

No comments