NAJUTA KUZALIWA MWANAMKE 03
NAJUTA KUZALIWA MWANAMKE 03
IMETUNGWA NA: Joshua Shao,
ILIPOISHIA………………………………………..
Jesca alitembea akinyata hadi nje ,alipofika nje aliona hali ni shwari kwa haraka aliendelea kutembea hadi geti la nje ili aweze kufungua na kutoroka
Mlinzi akiwa bafuni alikua akiimba kwa furaha sana alijiseme moyoni
``hahahah hapa leo Napata utamu pia napandishwa cheo maana lazima huyu ni mrudishe kwa mama shushu ,ukileta huruma kazini lazima ufe njaa’’
Mlinzi alivyomaliza kuoga alizama ndani ,alipokelewa na chumba tupu ,jesca hakuwepo ,alivyorusha macho sehemu alipoweka funguo hakuona kitu
Jesca alipambana kufungua kofuli ,alihisi kujikojolea kwani kila funguo aliyojaribu iligoma ,funguo zilikua zaidi ya ishirini kujua ni ufunguo upi utafungua ilikua ni mtihani jesca ,,aliendelea kupambana lakini wapi ,mikono ilitota jasho kwa hofu alikiona kifo kikiwa karibu kabisa
Upande wa pili Mlinzi alihisi alichanganyikiwa alitukana kwa nguvu sana ``huyu mwanamke leo naua na lazima nimshike tu najua kufungua kofuli lile si kazi rahisi’’ mlinzi alichomoka kwenda getini
Jesca alizishika funguo zile kwa haraka aligundua kitu ,funguo moja ilikua iking’aa zaidi ya nyingine alijua bila shaka ndio ,kwa haraka alichukua ufunguo ule na kupitisha
Kutoka lilipo geti hadi chumbani ilikua ni umbali wa dakika mbili jesca alibakiza dakika mbili za kuokoa nafsi yake
Jesca alipouingiza ufunguo hakuamini macho yake kofuli lile lilifunguka ,jesca kwa haraka sana alifungua mlango na kukimbilia nje ,akiwa anakimbia mlinzi nae alitokeza ,kwa hamaki alisema
``wewe mtoto subiri hapo nitakuua wewe’’
Jesca hakutazama nyuma alichapa mbuga kukimbilia sehemu za jirani ili aweze kupata msaada
Upande wa pili mama shushu aliitisha kikao cha dharura ,siku hiyo alikua na hasira kama simba ,alikua akitukana sana
``leo wapuzi nyie mmefanya uzembe wa kutosha haya yuko wapi jesca ‘’
Walinzi wote walitazamana kwa aibu kwani hakuna aliyekuwa na taarifa zake
Mama shushu aliuliza tena ``kimya mnamaanisha nini ok ngoja niwafanye kinachostahili ,abdulli njoo na timu yako wapeleke hawa wapuzi chumba cha mateso hadi watakapoweza kuongea naona sasa hivi wamekuwa mabubu’’
Mlinzi mmoja kusikia hivyo kwa haraka alijibu
``nilisikia mzee kirike akiwa anamkimbilia mtu getini pale nadhani itakua ni Yule msichana hivyo pelelezeni vizuri ‘’
Mama shushu kwa haraka alishuka kumfuatilia mzee kirike ili aweze kujua jesca yuko wapi ilikua ni kawaida ya walinzi kuwachukua wanawake waliokuwa wakiletwa pale kwa ajili ya kazi hivyo mama shushu alijua lazima jesca atakua akigawa penzi kwa mzee kirike , upande wa pili mzee kirike alikua akimkimbilia jesca kwani jesca alikua tayari amefanikiwa kuchomoka katika himaya ya mama shushu ,Jesca akiwa anakimbizwa ilifika hatua aliishiwa na nguvu kabisa ,miguu ilimuuma,mwili mzima alijihisi mzito ,jesca alitamani kukata tamaa ila kila akijaribu kukata tamaa alijipa moyo , alikimbia kwa nguvu zake zote, alipokua akivuka barabara nusura gari limgonge ,ashukuriwe Mungu mwendesha gari alikua na spidi ya taratibu ,kumbukumbu ya jesca ingefutika katika ulimwengu huu kwani kifo kilikua kilikua kimemnyemelea
Mwendesha gari alifunga breki kwa haraka na kushuka ndani ya gari lile kisha alimfuata jesca ambaye alikua chini
``wewe binti unashida gani wewe utatuletea kesi za kuua wewe mpuzi sana wewe ,huna akili kabisa ,msichana mrembo ila akili huna kabisa ‘’
Mwendesha gari akiwa anamfokea jesca mzee kirike aliyekua akimkimbiza jesca aliona hapa nikukimbia tu hana namna ,kirike alirudi kwa mama shushu akijiandaa kujibu mashtaka
Mwendesha gari alimsemesha jesca ``umetokea wapi wewe ‘’ huku akihema kwa nguvu jesca alijibu
``nilikua nimetekwa hapa nilipo nilikua nikikimbizwa ndio maana naomba msaada kama hutojali ‘’
Mke wa dereva Yule alishuka na kusogelea karibu ,walisikiliza maelezo ya jesca mwishoe waliona wamsaidie
``haya panda ndani ya gari ‘’
Jesca alifurahi sana alijua sasa amepona na atakuwa salama
Upande wa pili mzee kirike aliwasili katika himaya ya mama shushu ,mama shushu alipomwona alimuuliza kwa jazba
``wewe mpuzi umeamua kumtorosha huyu binti siyo’’
Mzee kirike huku akijitetea alijibu
``hapana sihusiki kwa lolote’’
Mama shushu hakuwa na muda wa kujadiliana na kirike
Alichomoa bastola kwenye kibegi chake cha mkononi na kumwasha ya kichwa
Mzee kirike alidondoka chini huku akisema
``mama shushu nimekua mtumishi wako mwaminifu leo umenilipa haya natamka haya Mbele za Mungu damu yangu itakufuatilia ,pia damu za mabinti wasio na hatia zitakufuatilia’’
Mama shushu alijibu kwa nguvu
``nyamazaaaaa mpuzi wewe ‘’ alimsogelea mzee kirike na kumwasha nyingine ya mdomoni
Mzee kirike alipoteza maisha pale pale ,, walinzi wa himaya ile hawakuamini kama mama shushu ni mnyama kiasi kila mmoja alimtazama mwenzake kwa mshangao ,mama shushu huku akijititimua alisema ``sasa yoyote atakayefanya uzembe kazini kifo kitamhusu nadhani wote mmemwona huyu nguruwe mwenzenu’’
Upande wa pili jesca alichukuliwa na kupelekwa kwa watu wale ,akiwa ndani ya gari aliulizwa maswali mengi ,jesca alijitahidi kujibu kama alivyoulizwa
Jesca aliingizwa katika nyumba kubwa ya kifahari ,alipofika alisikia sauti za watoto wakisema
``dad ,dad pole baba pole mama ‘’
Watoto waliwakumbatia wazazi wao kwa furaha
Jesca alitambulishwa kwa watoto pia wenyeji wake walijitambulisha baba Yule alianza kwa kujitambulisha
``mimi naitwa salum au waweza niita baba kenedy’’
Mama naye alijitambulisha ``mimi naitwa veronica ila waweza niita mama kenedy ‘’
Kwa upole jesca alijibu ``nashukuru kuwafahamu’’
``ok sawa jesca jisikie upo nyumbani karibu nadhani itakua vizuri ukae na sisi hapa uangalie watoto wetu wakati tukiangalia namna ya kukusaidia ‘’
``nitashukuru sana ‘’ alijibu jesca kwa sauti ya upole na kwa adabu
Ilipofika usiku wote waliketi sehemu ya kula kila mmoja alionekana mwenye furaha ,,wakiwa wanaendelea kula chakula cha jioni mama kenedy alioshangazwa sana na hali ya mumewe
Macho ya mumewe yalilala juu ya sura ya binti mgeni jesca ,muda wote salum alikua akimtazama jesca ,hakika jesca alikua ameumbika sana kiasi cha kumzuzua baba kenedy au salum
Mke wake alipoliona hilo kwa hasira alitoka nje na kwenda kuketi mbali kabisa akiwaza kwanini baba kenedy anakosa adabu alijisemea kwa nguvu
``khaaa huyu mwanaume si mtu, yaan hadi anajimwagia chakula nguoni ,kisa tu uroho wa kumtazama huyu binti, kwani mimi nina mapungufu gani daaah’’
Kitendo cha mama kenedy kutoka nje kilikua ni nafasi nzuri sana ya salum kumdodosa jesca maswali
Mama kenedy aliona usalama ni kumwonya jesca kabla hajaendelea kuishi pale kwani kitakachoendelea hakitakua ni kizuri.
Baada ya chakula wote walitawanyika kwa ajili ya mapumziko ,mama kenedy aliongozana na jesca hadi chumba kilichotengwa kwa ajili ya wageni alipomfikisha alimwambia
``mama jisikie amani pumzika hapa ;’’
``asante mama ‘’
``ila nakuomba uwe makini mume wangu si mwaminifu sana hivyo ukiona analeta mazoea ya ajabu muepuke au uniambie’’
``sawa mama ‘’ jesca alijibu huku akiagana na mama kenedy
Jesca aliingia kitandani alizima taa yake na kumshukuru Mungu hakuamini kama leo angekua mahali salama
Upande wa pili salum au baba kenedy aliwaza sana juu ya mtoto jesca ,alijaribu kulala ila usingizi ulimruka kabisa hakuwa na hata lepe la usingizi ,alipomtazama mkewe alimwona mkewe amechapa usingizi ,taratibu aliamka huku akinyata alitoka na kuelekea chumba cha wageni aliko jesca
Jesca akiwa amelala alisikia mlango wake ukiguswa ,jesca alishtuka sana kwani hakujua ni nini
Jesca alipotazama alimwona salum akiwa mbele yake akiwa amevalia bukta na sing’lendi nyeupe
``samahani sana najua umeogopeshwa na mimi kuwa hapa ,mapenzi yameujaza moyo wangu nimeshindwa kulala bila kukuona wewe naomba unipe nafasi ya kuwa nawe hata kwa nusu saa nitakulinda na kukufikisha kwenu salama ‘’
Jesca alitetemeka hakuwahi kuamini kama kitu kama kile kitamtokea ,kwa haraka alikumbuka maneno ya mama kenedy mke wa salum `` nakuomba uwe makini mume wangu si mwaminifu sana hivyo ukiona analeta mazoea ya ajabu muepuke au uniambie’’
Jesca alijikuta akishikwa na kigugumizi akisema ``sii-weziii-nisamehe-bure’’
Salum alisogea hadi kitandani na kuketi karibu nae
Upande wa pili mama kenedy alizinduka usingizini ,alipotazama pembeni hakumwona mume wake ,kwa haraka alikurupa na kutoka ndani alijua hapa kuna kitu kinaendelea siyo kawaida
Je nini kinaendeleaa…………………..
Share like na comments
No comments