NAJUTA KUZALIWA MWANAMKE 02
NAJUTA KUZALIWA MWANAMKE (2)
ILIPOISHIA…………………………….
Mlinzi alimparamia jesca kwa haraka mithili ya mtu amenyavyo ganda la ndizi ,baada ya kuzivua nguo zake alimwingilia jesca ,jesca alilia sana kwa uchungu kwani ndio mara yake ya kwanza kufanya tendo lile ,alijisikia vibaya sana ila kwa usalama wa maisha yake alikua radhi kugawa mwili wake ili apone
Baada ya nusu saa kuisha jesca alimwuliza mlinzi
``naomba unitoe tafadhali ‘’
Mlinzi alicheka hahahah nikutoe wapi hahaha ulishasikia mtu ameingia hapa na kutoka ‘’
Jesca hakuamini kitu mlinzi alichomfanyia ,,,,jesca alijisemea
``Mungu wangu nimejidhalilisha nimempa huyu hadi heshima yangu aninusuru ila matokeo yake ndio haya ,,’’
Mlinzi alisema
``wewe una dakika tano za kukaa hapa natakiwa kukurudisha ndani ‘’
Jesca kwa hasira aliinama chini na kuokota chupa ya bia iliyokuwa ukutani na kumpasulia mlinzi kichwani ,,mlinzi alishikwa na kizungu zungu na kudondoka chini
Jesca akiwa amesimama eneo hilo alisikia vishindo vya watu wakiwa wanakaribia ndani ya kijumba kile
Jesca alihisi kuchanganyikiwa mlinzi Yule alikua chini akiwa amepoteza fahamu,hii ni kutokana na chupa aliyopigwa kichwani na jesca ,jesca akiwa anaendelea kubabaika akiwa hajui lipi la kufanya
Alisikia sauti za vishindo vya miguu ya watu vikiendelea kukaribia jumba lile ,jesca alihisi kuchanganyikiwa kwani alijua hapa kinachofuata ni kifo tu alikumbuka asubuhi dada yake alivyouawa kikatili na watekaji wale ,,,jeska akiwa anaendelea kuwaza na kuwazua kwa mbali aliona mwanga ,kwa haraka alibaini lazima kutakua na kijimlango au dirisha katika nyumba ile ,
Jesca alikimbilia upande ule na kweli ilikua kama alivyowaza kulikua na kidirisha kidogo ,jesca alimshukuru Mungu kwani angetorokea upande wa mbele walikoingilia lazima ashikwe
Upande wa pili mama Yule kibonge ajulikanae kama Mama shushu aliwasili majira ya saa tatu akiwa na matajiri wake ambao kila siku jioni lazima wawasili pale kwa ajili ya kujituliza na vimwana na mademu wakali waliokuwa pale
Mama shushu leo aliwaleta matajiri kifua mbele kwani alikuwa ameshawapa taarifa kuwa leo kuna kimwana mpya mbichi mbichi mwenye umbile linaloweza kutoa nyoka pangoni ,mama shushu alitia chumvi sana alipokuwa akimsifia jesca aliwaambia matajiri wale
``haaa huyu msichana ni mrembo kupindukia shepu yake ni nane baba kifuani je usiseme ,,anavutia nadhani mkimwona nadhani mtatoa udenda wenyewe ‘’
Matajiri wale walifurahi na kukimbilia kwa furaha kwenda kumtazama jesca ili waweze kupanga bei ya kulala nae ,,,kwa kifupi hiyo ndio ilikua kazi ya mama shushu ambayo ilimpa utajiri na mafanikio makubwa sana
Mama shushu alivyowafikisha matajiri wale aliwapa vinywaji na kwa haraka alikimbilia sebuleni alipomwacha jesca kwa ajili ya kumchukua na kumpeleka kwa maboss wale
Mama shushu alipofika sebuleni hakuamini macho yake kwani jesca hakuwepo ,kwa panic na hasira alitoka hadi nje kwa mlinzi ,cha kushangaza hata mlinzi hakuwepo
Mama chuchu alihisi kuchanganyikiwa alimwaga matusi kwa hasira alisema
``hawa wapuziii ,washenzi leo nafukuza kazi wote hemedy yuko wapi na huyu jesca niliyemleta yuko wapi’’
Mama shushu aliwaagiza wote wazunguke jingo lile kumtafuta jesca
Vijana wa kazi walitapakaa kila kona kumtafuta jesca
Upande wa pili jesca alikua akipambana kupenya katika dirisha lile kwa nje aliona uzio wa seng’enge alijisemea ``nikiweza kutoka hapa lazima nitapata usaidizi
Hatimaye jesca alifanikiwa kuruka juu ya dirisha na kudondokea nje
Alipodondoka tu kishindo kikubwa kilisikika ,kilichomzindua mlinzi wa geti la nyuma ,
Upande mwingine walinzi waliweza kufika ndani ya kijumba kile ,walimkuta mlinzi akiwa chini huku damu zikimtiririka ,kwa haraka taarifa zilifika kwa mama shushu ,mama shushu mkuu wa kambi ile ,aliamuru mhalifu akamatwe ,ulinzi uliendelea kuimarika watu waliendelea kutafuta huku wakijiami zaidi kwani walihisi kuna watu wa tofauti ndani mule ,laity kama wangejua kuwa ni jesca mwenyewe kafanya vile
Kishindo cha jesca kilimwamsha mlinzi ,kwa haraka mlinzi aliwasha tochi ,maskini jesca alionekana wazi wazi akiwa anapambana kuvuka uzio
Mlinzi alishuka moja kwa moja na kumfuatilia jesca
Jesca kama kawaida yake alipiga magoti chini na kulia sana ``baba nisaidie mwanao ,nisaidie kutoka hapa usinirudishe tafadhali ‘’
Mlinzi Yule alicheka na kusema
``hahahaha unasikia kelele zote huku juu ni wewe unatafutwa tu ,na kwa taarifa yako sisi tutafukuzwa kazi wote endapo hautapatikana ‘’
Jesca aliendelea kumbembeleza huku akisema
``nitakupa chochote baba yangu ‘’
Mzee Yule alirusha macho kwenye mwili wa jesca ,,,,alijikuta akiingiwa na matamanio makubwa kwa jinsi jesca alivyo mzuri ,mzee Yule alijikuta akitafakari maneno ya jesca ``nitakupa kitu chochote baba’’
Mzee Yule alisema
``uko radhi kulala na mimi usiku huu alafu nikutoroshe hapa’’
``niko tayari baba’’ jesca alijibu kwa haraka bila hata kufikiria
Mzee Yule kwa haraka alimwambia jesca njoo hivi alimpeleka ndani ya kijumba Fulani kisha alianza kumwelezea jesca
``wewe unaonekana ni binti mdogo kabisa ,nikikuona na mkumbuka binti yangu ‘’
``hahah asante baba’’
``daaah tabasamu lako ndio kabisa kama mwanangu ,,,ila unajua mimi sikutaka kufanya kazi kama hii ya kulinda kambi ya namna hii ,sema uhaba wa pesa nimejikuta nikiajiriwa na mama shushu ,kila mara mabinti hutekwa na kuletwa hapa wanazalisha hela kwa kutumika kingono ,hili linaniuma sana na sijui nitaenda kutubu wapi hii dhambi’’
``pole baba angu ‘’ jesca alimwambia
Jesca kwa haraka alipomwangalia mzee Yule aliweza kugundua kuwa mzee Yule ni mwema ila akili zake zilimwambia ``itakuaje kama nitatoa tena penzi alafu niachwe bila chochote au niambulie kurudishwa kwa mama shushu’’
Mzee Yule aliendelea
``njoo basi huku natamani tuwe karibu si umekubali mwenyewe kunipa penzi au haupo tayari nikurudishe ‘’
``nipo tayari ila naomba unielekeze utanitoa kwa njia ipi hapa kambini baba ‘’
``ohoooo kuna mlango ambao uko nyuma ya uzio sijui kama unaujua ‘’
Kwa haraka jesca alikumbuka
``ndio nimeuona ;;’
``sawa funguo zake zile pale tutaenda nikufungulie unatoka kiwepesi bila hata makelele wala shida
Jesca jicho lake alilitupa juu ya mlango aliziona funguo zile ,taratibu alimfuata mlinzi alimshika na kumkiss,mlinzi alijisikia kuchanganyikiwa na umri wake mambo hayo nikitambo hajawahi yapata ,
Jesca aliongea kwa sauti ya kimahaba
``baba unaonaje tukaoga kwanza ndio tukaendelea ,ndani ya chumba nimeona bafu la ndani itawezekana ‘’
``hahaha mrembo samahani najua natoa harufu mbaya ila ndio hivyo kazi zetu lazima tuwe wachafu’’
``usijali bwana we kaoge alafu uje utanikuta hapa ‘’
Mlinzi alipagawishwa na busu taratibu alijikuta akinyanyuka kuelekea bafuni aoge ndipo aje rasmi kuendelea na shughuli nzito
Mlinzi alipofika bafuni jesca alinyanyuka na kuchukua funguo zile ,alijisemea
``hapa nikifanya uzembe sina bahati ‘’
Jesca alitembea akinyata hadi nje ,alipofika nje aliona hali ni shwari kwa haraka aliendelea kutembea hadi geti la nje ili aweze kufungua na kutoroka
Mlinzi akiwa bafuni alikua akiimba kwa furaha sana alijiseme moyoni
``hahahah hapa leo Napata utamu pia napandishwa cheo maana lazima huyu ni mrudishe kwa mama shushu ,ukileta huruma kazini lazima ufe njaa’’
Mlinzi alivyomaliza kuoga alizama ndani ,alipokelewa na chumba tupu ,jesca hakuwepo ,alivyorusha macho sehemu alipoweka funguo hakuona kitu
Jesca alipambana kufungua kofuli ,alihisi kujikojolea kwani kila funguo aliyojaribu iligoma ,funguo zilikua zaidi ya ishirini kujua ufunguo upi utafungua ilikua mtihani jesca ,,aliendelea kupambana lakini wapi ,mikono ilitota jasho kwa hofu alikiona kifo kikiwa karibu kabisa
Mlinzi alichanganyikiwa alitukana kwa nguvu ``huyu mwanamke leo naua na lazima nimshike tu najua kufungua kofuli lile si kazi rahisi’’ mlinzi alichomoka kwenda getini
Jesca alizishika funguo zile kwa haraka aligundua kitu ,funguo moja ilikua iking’aa zaidi ya nyingine alijua bila shaka ndio ,kwa haraka alichukua ufunguo ule na kupitisha
Kutoka lilipo geti hadi chumbani ilikua ni umbali wa dakika mbili jesca alibakiza dakika mbili za kuokoa nafsi yake
Je nini kitaendelea
Je jesca atapona ,mama shushu ana lipi la kufanya ,mlinzi je ataweza kumkamata jesca
No comments