ISABEL DOS SANTOS MWANAMKE TAJIRI AFRIKA ATUHUMIWA KULIPORA TAIFA LAKE
MWANAMKE tajiri zaidi Afrika, Isabel dos Santos amefunguliwa mashtaka ya ulaghai baada ya kutuhumiwa kulipora taifa hilo.
Mwanasheria Mkuu, Helder Pitta Groz alisema kwamba madai hayo yanahusiana na wakati alipokuwa mwenyekiti wa kampuni ya mafuta ya Sonangol.
Watu kadhaa pia wametuhumiwa pamoja na Isabel.
Groz alisema kwamba wataomba kibali cha kimataifa cha kuwakamata iwapo watagoma kujikabidhi wenyewe mbele ya mamlaka ya Angola.
“Isabel dos Santos anatuhumiwa kwa usimamizi na ufujaji wa fedha wakati alipokuwa mwenyekiti wa kampuni hiyo ya Sonangol, hivyo basi amefunguliwa mashtaka ya usimamizi mbaya wa ofisi, kutumia ushawishi wake na kughushi stakabadhi miongoni mwa uhalifu mwengine wa kiuchumi,” Groz aliuambia mkutano na wanahabari Jumatano jioni.
Alisema uchunguzi kuhusiana na usimamizi wake wa kipindi cha miezi 18 katika kampuni hiyo ya mafuta kuanzia Juni 2016, ulianzishwa baada ya mrithi wake, Carlos Satumino kuelezea mamlaka kuhusu uhamishaji wa fedha usio wa kawaida.
Stakabadhi zilivuja wiki hii zikidai kwamba Isabel, mwana wa aliyekuwa rais wa taifa hilo, Jose Eduardo dos Santos, alijipatia mali ya thamani ya dola bilioni 2.1 kwa kulipora taifa lake.MWANAMKE tajiri zaidi Afrika, Isabel dos Santos amefunguliwa mashtaka ya ulaghai baada ya kutuhumiwa kulipora taifa hilo.
Mwanasheria Mkuu, Helder Pitta Groz alisema kwamba madai hayo yanahusiana na wakati alipokuwa mwenyekiti wa kampuni ya mafuta ya Sonangol.
Watu kadhaa pia wametuhumiwa pamoja na Isabel.
Groz alisema kwamba wataomba kibali cha kimataifa cha kuwakamata iwapo watagoma kujikabidhi wenyewe mbele ya mamlaka ya Angola.
“Isabel dos Santos anatuhumiwa kwa usimamizi na ufujaji wa fedha wakati alipokuwa mwenyekiti wa kampuni hiyo ya Sonangol, hivyo basi amefunguliwa mashtaka ya usimamizi mbaya wa ofisi, kutumia ushawishi wake na kughushi stakabadhi miongoni mwa uhalifu mwengine wa kiuchumi,” Groz aliuambia mkutano na wanahabari Jumatano jioni.
Alisema uchunguzi kuhusiana na usimamizi wake wa kipindi cha miezi 18 katika kampuni hiyo ya mafuta kuanzia Juni 2016, ulianzishwa baada ya mrithi wake, Carlos Satumino kuelezea mamlaka kuhusu uhamishaji wa fedha usio wa kawaida.
Stakabadhi zilivuja wiki hii zikidai kwamba Isabel, mwana wa aliyekuwa rais wa taifa hilo, Jose Eduardo dos Santos, alijipatia mali ya thamani ya dola bilioni 2.1 kwa kulipora taifa lake.

No comments