MATOKEO YA UCHAGUZI WA CHADEMA
Katika mlolongo wa uchaguzi uliokuwa ukiendelea chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA, katika ukumbi wa mlimani city. Hatimaye siku ya jana ilikuwa ni siku ya kuchagua viongozi wakuu wa chama kitaifa. Nafasi ya mwenyekiti taifa ilikuwa na wagombea wawili, mh. Freeman Mbowe na mh. cecil David Mwambe.
Katika nafasi ya makamu mwenyekiti ilikuwa na wagombea watatu mmoja akigombea nafasi ya Zanzibar ambaye ni mh. Said Issa Mohammed. Nafasi ya Tanzania bara ilikuwa na wagombea wawili mh. Tundu Antiphas lissu na mh. Sophia Hebron Mwakagenda
Wajumbe wa kamati kuu walipiga kura kwa demokrasia yote na kwa amani na kisha kuchagua viongozi waliowachagua
MATOKEO
Makamu zanzibar MH. SAID ISSA MOHAMMED kuwa za ndio ni 836 hapana ni 95
Makamu Tanganyika. TUNDU LISSU KURA 930
MH. FREEMAN MBOWE KURA 886 CECIL MWAMBE KURA 59
Hivyo FREEMAN MBOWE ataendelea kuwa mwenyekiti kwa miaka mitano zaidi pamoja na makamu wake Tundu Lisu kwa Tanzania Bara na makamu wake Said Issa Mohammed kwa Zanzibar.
No comments