MAMA ACHINJWA, MTOTO ANYONGWA


mwanamke aliyefahamika kwa jina la Vaileth Mafunda (21) mkazi wa Mtaa wa Vuta, Kijiji cha Kizwite, Manispaa ya Sumbawanga, ameuawa kwa kuchinjwa na huku mtoto wake mwenye mwaka na nusu akinyongwa, na maiti zao kutupwa nje ya nyumba ya mjomba wake.
Akizungumzia tukio hilo, mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Vuta, Milton Boniface, alisema tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia juzi ambapo watu wasiojulikana walidaiwa kufanya mauaji hayo.
Boniface alisema asubuhi ya siku hiyo walipata taarifa kutoka kwa majirani kuwa kuna mwanamke kauawa kwa kuchinjwa akiwa na mtoto wake mgongoni ambaye anadhaniwa kuwa naye alinyongwa katika tukio hilo la mauaji.
Alisema baada ya taarifa hizo, walifika eneo la tukio na kukuta maiti ya mwanamke ikiwa imechinjwa na huku akiwa amevuliwa sketi na nguo za ndani, huku akiwa amebeba mtoto mgongoni ambaye naye alikuwa amefariki dunia.
Walipoukagua mwili huo walibaini kuwa ni wa Vaileth ambaye ni mkazi wa mtaa huo na kisha kutoa taarifa polisi ambao walifika na kuchukua miili hiyo kuifanyia uchunguzi.
Mjomba wa marehemu, Kefas Lemizio, alisema walipoamka asubuhi waligongewa na jirani yao na kuambiwa nyuma ya nyumba yake kuna maiti ya mpwa wake.

No comments

Theme images by jangeltun. Powered by Blogger.