NAJUTA KUZALIWA MWANAMKE 08


Hussein akiwa njiani mbele yake aliona watoto wawili wakiwa wanacheza barabarani ,Hussein alipiga honi kuwataka waondoke ila watoto wale waliendelea kutanga tanga wasijue wanaenda wapi
Hussen alijitahidi kuwakwepa kwa kila namna ila alishindwa ,gari la Hussein liliwavaa watoto wale na kuwasagasaga ,kisha lilipinduka mara tatu ,si husseinsi watoto wote walikufa
Watu walikimbilia mahali pale ,wasamaria wema walijitahidi kuwasaidia ila huwezi amini Hussein alipoteza maisha pale pale ,,,,,,pembeni ya gari simu ya Hussein ilionekana baba mmoja aliichukua ,kwa haraka aliona namba imeseviwa  MKE WANGU’’ waliichukua na kupiga simu , kwa bahati nzuri simu iliita
Jesca akiwa ndani anafanya usafi aliona simu yake ikiita ,alivyoona jina MUME WANGU aliachia tabasamu la nguvu
Jesca kabla hajapokea aliibusu simu ile huku akisema
``mhhhh baby wangu ushanimiss mapema hii duuuuh’’
``hellow naongea na mke wa hussein’’
``hellow baba umefika salama ‘’ jesca aliongea kwa haraka akidhania anaongea na laazizi wa moyo ‘’
Alipoendelea kusikia sauti ile alishtuka sana kwani ilikua si sauti ya Hussein ,aliwaza kwa haraka simu ya Hussein itakua imeibiwa nini
``hellow mimi ni mke wa Hussein naongea na nani tafadhali’’
``unaongea na mzee sumbai hapa samahani kuna tatizo kidogo limejitokeza ‘’
``duuuuh tatizo gani jamani ,mume wangu si tumeagana hapa’’
``unajua bwana Hussein kwa sasa…..’’
Kabla hajamalizia kusema mzee mmoja alimpokonya mzee sumbai simu na kumwambia ``utakuja kuua watu wewe acha upuuzi taarifa za kifo hazitolewi kama mtu anatoa kamasi’’
Simu ilikatwa
Jesca alihisi kuchanganyikiwa alizunguka kila mahali si sebuleni si chumbani hakujua ni nini kimempata mume wake ,jesca alitamani kutoka kwenda kazini kwa bwana ake akakumbuka njia wala haifahamu
Ndani ya dakika kumi simu ilipigwa upande wa ndugu za Hussein
Jesca aliona simu ya wifi yake yaan dada wa Hussein aliyekuwa akiitwa cathe ,kwa haraka alipokea
Cathe alikua akilia sana ,kupita maelezo
``mhhh wifi mbona unalia ‘’
``Hussein…..ameku…fa’’
Jesca aliposikia hivyo alidondoka chini moja kwa moja na kuzimia
Cathe aliendelea
``hellow ,hellow ‘’
Alisikia kimya ila simu ilikua hewani tu
Cathe pamoja na mama mzazi wa Hussein pamoja na kaka walichukua gari kuwahi nyumbani
Walipofika walimkuta cathe akiwa chini
Walianza kumpulizaa
Kilio kilitanda kila mmoja alikua akilia kivyake mama mzazi wa Hussein alikua akisema
``mwanangu uliniahidi muda si mrefu utaniletea kajukuu ka kike tena ukape jina langu mimi ,mwanangu naamini haujafa zinduka mwanangu’’
Walilia sana ,baadhi ya wana familia walitangulia mochwari kuhakiki kama kweli mwili ule ni wa Hussein ,hakika ilikua ndivyo kabisa ,Hussein alikufa kifo kibaya gari lilimsagasaga kabisa si miguu si mikono alisagika hii iliwahuzunisha sana ,kilichowasikitisha sana watu ni baba mzazi wa Hussein kusema
``mwanangu ulikua mkarimu ,mwanangu ulikua mtu wa watu ,umenisaidia mimi umesomesha wadogo zako ,mwanangu pumzika kwa amani ,ila Mungu kwanini umemwacha mja wako afe kifo kibaya namna hii ,sia ngeumwa hata malaria afe sasa baba anakufa kwa ajali ‘’
Kila mtu hadi wafanyakazi wa mochwari waliangua kilio ,aseee kuna mambo yanauma katika maishaa lakini siyo kama kuondokewa na mtu wa karibu umpendae
Upande wa pili jesca alizinduka ,alipozinduka aliwaona wifi zake pamoja na mama mkwe wake wakiwa wameshikilia picha ya Hussein huku wakilia
Jesca  kuona hivyo alizimia tena
Mama mkwe alijikuta akishikwa na hasira aliropoka vibaya
``huyu kahaba anatuongezea kazi ya kumpepea kila saa kuzimia au anajikuta yeye alimpenda mwanangu zaidi ya mimi mama yake mpuuzi kabisa huyu ,cathe mwanangu usimpepee huyu mbwa huyu’’
Cathe alimziba mama yake mdomo kwani mama yake aliongea maneno ya kishetani kabisa ambayo jesca angeyasikia angeweza kufa afuatane na bwana ake
Cathe alimpepea wifi yake tu hadi alipozinduka tena
Taratibu za mazishi ziliendelea ,msiba wa Hussein ulikua ni pigo kubwa sana ,,,ilipofika siku ya mazishi  ,,watu walifurika jesca alilia sana ,ndugu jamaa na marafiki walilia sana
Wakati wa wosia wa marehemu  kusomwa watu walitulia kimya kusikiliza ,kilichowashangaza watu pamoja na jesca ni hiki
Iliposomwa wosia waliandika ``Marehemu amefariki akiwa hana mtoto wala mke’’
Jesca alihisi kuchanganyikiwa alijisemea ``mhhh itakuwaje kwa hiyo mimi siyo mke wa hussein’’
Jesca aliamua kupotezea ,pole zilitolewa ,watu walimruka jesca hakuna aliyemjali jesca kama mfiwa ,,,jesca alimuuliza wifi yake ajulikanae kama cathe
``wifi angu mbona mimi sitambuliki kama mke jamani  au kuna kitu gani jamani nijue’’
mhhhh pole mama ndio wameamua hivyo sina la kukusaidi’’
Baada ya msiba kuisha kila ,,habari za Hussein zilisahaulika
Kutokana na hussein kuwa na hela nyingi ,majumba na magari pale mjini ,ndugu zake waliamia mjini ,ikiwa ni pamoja na mama baba na cathe dada wa Hussein
Siku moja asubuhi kama ilivyokuwa kawaida ,jesca mke wa marehemu aliamka na kwenda sebuleni
Aliichukua picha ya Hussein na kuibusu huku akitamka
``mume wangu mpendwa naamini ulipo upo mahali salama ,naahidi kutunza na kukileta kichanga duniani ,kama ulivyoniambia huyu ataitwa happy ,furaha ya ulimwengu ,hivyo na kuahidi kutimiza ‘’
Jesca akiwa anasema hayo mama mkwe  wake alikua nje kidogo alisikia yote ,kwa haraka alifunga kanga yake vyema nakuingia sebuleni
``wewe kahaba funga bakuli lako ,mchawi mkubwa wewe ,unasema unamimba ya mwanangu ,Malaya wewe uliyeokotwa sijui hata kijana wangu alikupendea nini wewe kisura chako cha kikahaba kabisa ‘’
Maneno yale yalizama kama msumari wa moto moyoni mwa jesca ,jesca alihisi kuishiwa nguvu ,,,,,picha ya Hussein ilimchomoka na kudondoka chini
Mama mkwe aliendelea kuropoka
``kahaba wewe unaona hadi picha ya mwanangu ina kukimbia hahahah nikifumba macho na kufumbua ……’’ kabla hajamaliza kusema baba mkwe wa jesca aliingia na cathe
Je nini kitaendelea……………………….
Jesca bado hali ni tete ,,nini mwisho wa binti huyu

No comments

Theme images by jangeltun. Powered by Blogger.