KUSUKUMWA NA UPENDO 3
Hadithi=> KUSUKUMWA NA UPENDO
Sehemu ya : 3 ***msituni
“Namna gani kuhusu mipango ya mifugo, inakwendaje”? nilimwuliza. “ Inaendelea vizuri. Wiki jana nilikuwa na wasiwasi kwa sababu baadhi ya ng’ombe juu mlimani walipata ugonjwa. Kwa kweli mmoja alikufa. Nilifikiri nitalazimika kufanya kazi ile yote peke yangu kuwatunza wapate afya tena. Lakini mipango maalumu ilifanyika. Watemi walishughulika wenyewe na mambo haya. Waliwapa dawa nzuri na waliwatunza ng’ombe mpaka walipona. Sasa wanatoa maziwa mazuri sana.“ Bobby aliinama mbele na kunitazama kwa werevu. “Kwa kweli Bruchko, tulikuwa na maziwa mengi kupita kiasi kule Iquacarora kiasi kwamba yalianza kuharibika. Kwa hiyo tuliyawahi tukatengeneza jibini.” “Nini? mlitengeneza kwa njia gani?” Alionyesha mshangao. “Tulitengeneza jibini kwa njia rahisi, kwa njia ya kawaida inayotumiwa na watu wote.” Alianza kucheka. Nilifahamu kwamba nilikuwa na mtazamo wa mshangao. “Tulitumia dawa ile ile uliyoiacha kwetu. Tulisoma maelekezo jinsi ya kufanya. Na ilitokea vizuri sana. Unaweza kupokea kidogo mwenyewe tukifika Iquacarora ikiwa hawajaimaliza.”
Niliketi nikishangaa. Miaka kumi zamani Bobby alikuwa mvulana mzuri tu mwenye kicheko cha ajabu. Sasa alikuwa kiongozi wa watu wake. Labda kazi ya kutengeneza jibini haikuwa kubwa sana. Lakini alionyesha ya kwamba Wamotilone walikuwa hawana kiongozi. “Bobby” nikasema, “sasa u kiongozi wa watu wako, ni madaraka makubwa.” Aliinua mabega yake. “Si mimi tu. Kuna watu wengine wengi ambao wanaweza kushika madaraka kama haya na kufanya vizuri sawasawa na mimi. Zaidi ya hayo Bruchko, Yesu Kristo anajua tunahitaji nini. Ikiwa hatutamdanganya au kusema uongo, atakuwa kiongozi wetu kweli kweli.”
Bobby akasema: “Bruchko ungeona shule zetu, zimejaa wanafunzi. Wengi wao wamemaliza kusoma vitabu tulivyovitafsiri na wanataka kupokea vitabu vingine. Zaidi vitabu vya agano jipya. Wanazungumza juu ya mambo ambayowanajifunza kama vile watu wanavyozungumza juu ya mbinu za uwindaji. Wazee wetu nao wanafanya vilevile.Ni lazima tufanye kazi ya kutafsiri maandiko zaidi kwa ajili yao , la sivyo hatutakuwa na amani’’.
Nilicheka. ’’ Sawasawa. Tutaanza kazi hii upesi iwezekanavyo. Sasa itakuwa rahisi zaidi baada ya kufaulu kutafsiri maneno magumu zaidi kwanza.” Matazamio ya kutafsiri zaidi yalinifurahisha, kwa sababu nilijifunza maneno mengi kutoka Biblia kuhusu kazi hii. Nilifikiri juu ya neno “imani” kwa lugha ya Kimotilone ambalo lina maana kwamba: nimeunganishwa kwa mungu, sawasawa na jinsi Wamotilone walivyotundika wavu wa kulalia katika nyumba zao. “Kuunganishwa na Yesu” tunaweza kupumzika na kulala usingizi na hatimaye, kuimba huko juu bila hofu ya kuanguka.
“Nafurahi sana kuwa hapa tena pamoja nawe, Bobby”, nikasema. “Nilikukosa wakati wote nilipokuwa mbali. Nafikiri mimi nimeunganishwa na wamotilone.” “Na sisi tumeunganishwa na wewe. Bruchko”! Mtumishi alituletea kahawa yenye nguvu nay a moto sana. Bobby, alipokuwa akiikoroga hiyo kahawa, kicheko chake kilitoweka akanuna.`
Tumepata matatizo zaidi sasa na wajenzi [wakaaji] wapya. Wametutumia barua nyingi zenye dalili ya chuki na zenyevitisho.
Tangu zamani tumekuwa na matatizo na wageni hawa. Wengine kati yao walikuwa wamefungwa ambao walitoroka magereza na ambao waliishi ili wasikamatwe tena,
Walijaribu kuchukua nchi kutoka kwa Wamotilone ili waitumie kwa kulima mashamba yao na walitangaza nchi ile kama mahali pao pa usalama.
“Wanataka nini sasa?” niliuliza. “Unajua. Wanataka nchi zaidi. Wanaitaka zaidi nchi yetu. Wanatutendea kama wanyama wanaofukuzwa kwa kuwindwa kama apendavyo mwindaji.” Kwa hiyo unatazamia matatizo zaidi kutoka kwao, au wanatutisha tu? Sijui Bruchko, labda yaweza kuwa matatizo kweli. Inaonekana ya kwamba wageni wengi wamechagua upande wa watoro. Ina maana kwamba watoro kamwe hawatapokea nchi bila msaada wao.
“Sasa utafanya nini Bobby?”
Uso wake ulionyesha huzuni na alitazama chini. “Naweza kukuambia neno moja - ya kwamba sisi hatutaweza kuwapa kuwapa nchi zaidi. Mara kwa mara tumewapa na bado wanataka. Safari hii lazima tujilinde.” “Lakini Bruchko”, huku akinitazama, “natumaini na kuomba kwamba isiwe hivyo.”
Nilikuwa na wakati wa kutosha kufikiri juu ya neno hili tulipopanda mashua mtoni. Ulikuwa mwendo wa masaa saba na kwa sababu ya muungurumo wa mashine hatukuweza kuzungumza. Ilitusahangaza sana kwamba wageni walitusumbua tena. Jambo hili lilikuwa na nyuso mbili, zaidi ya wageni elfu tatu walitibiwa na Wamotilone katika nyumba zao za dawa.
Walipenda kuja kwetu walipohitaji msaada. Wamotilone waliwapa dawa na matibabu. Lakini walipoitaka nchi ya wamotilone wageni walijaribu kwa njia zote ili kuipata.
____ITAENDELEA____
No comments