AKIPENDA, CHONGO HUITA KENGEZA
'Chongo' hapa ni jicho lisiloona, na kengeza ni lile jicho linaloona, lakini limekaa upande upande.
Methali hii hupigiwa mfano yule mtu ambaye, anapolipenda au anapoliunga mkono jambo fulani au mtu au kitu fulani huwa hakubali kuwalina aibu au kasoro yoyote hata ikiwa kweli linayo basi atalitetea kwa kila namna. Badala ya kusema linayo kweli aibu fulani (au chongo) yeye atasema lah! Wewe huoni vizuri. Hiyo si aibu ni kasoro ndogo (ni kengeza) tu
No comments