NAJUTA KUZALIWA MWANAMKE 06


NAJUTA KUZALIWA MWANAMKE 6

Upande wa pili baba kenedy alikimbiza gari huku akiwa anacheka sana na mkewe
Walipofika mbele kidogo kwenye kilima kirefu ,gari lao liliacha njia na kuanza kuserereka ,mama kenedy alipiga kelele kubwa
``baba kenedy shika breki mpuzi wewe tutakufa eti ‘’
Baba kene alishika breki ,huwezi amini breki zilikataa katakata ,,gari iliendelea kuserereka
Mama kenedy alisema ``baba kene gari likidumbukia kwa korongo lile hatuponi’’
Kabla hajamalizi sentensi gari lilibinuka mara tatu hadi korongoni ‘’
 Baba kenedy alipoteza maisha pale pale ,mama kenedy alikatika katika mikono na miguu ‘’
Kwa haraka watu waliwasili pale na kumchukua mama kenedy kumwaisha serena hospital
Baba kenedy alipelekwa moja kwa moja mochwari kwani  alikua ni marehemu ,mama kenedy aliwahishwa chumba cha wagonjwa mahutihuti
Jesca akiwa kitandani anafanyiwa matibabu alisikia madaktari wakisemezana
``jamani kazaneni kuna ajali imetokea mmoja kafa ila mama ni mahutihuti kaletwa humu ,,,hali yake ni mbaya ‘’
``daaah ni ajali ya nini hii ‘’
``ya gari limepindukia hapo kwenye korongo la muleba bar’’
``daaah ‘’
Jesca alishtuka sana alijisemea
``Mungu wangu usikute ni mama kenedy na baba kenedy tu ,,,,Mungu epusha hawastahili kupata adhabu hiyo mbaya namna hii’’
Jesca akiwa kitandani dokta alimuuliza
``jesca mbona kama umeshtuka ‘’
Kabla jesca hajajibu alimwona mama kenedy akiingizwa chumba cha mahutihuti akiwa juu ya machela
Jesca alimwonea huruma sna alijisemea ``hakika mungu nimeogopa ukuu wako wamepata sawa sawa na waliyonitendea ‘’
Jesca aliendelea  kufanyiwa matibabu chini ya uangalizi wa daktari Hussein ,kijana Hussein alipambana sana na jesca alidiriki kununua chakula kwa ajili ya jesca kwani jesca hakuwa na mtu wa karibu ambaye aliwezakumhudumia
Siku moja asubuhi nesi  mmoja alimuuliza jesca
``hivi wewe nawe daktari Hussein tu ndio anaingia mfukoni kukutafutia chakula huna ,mtu mwingine ambaye anaweza kukusaidia wewe  ni wawapi kwanza???
Jesca huku akilia alimweleza nesi Yule mkanda mzima mwanzo hadi mwisho
Nesi alimwonea huruma sana jesca ,nesi subira naye aliungana na daktari Hussein kumsaidia jesca
Siku mbili zilkatika upande wa pili mtaani kila mahali kelele zilisikika
``ama kwelii maisha haya usimtendee mtu vibaya ,baada ya kumtelekeza Yule binti ndio mabaya haya yamewakuta  leo baba mtu kafa mama nae yupo hoi bin taaban ama kweli Mungu si wa mchezo mchezo siku zote tutende mema kwa kweli’’
Mambo yaliowakuta baba kenedy na mama kenedy yalikuwa fundisho kwa kila mtu mtaani pale
Zilipoo katika b siku tatu baba kenedy alizikwa ,mama kenedy hakuweza kabisa kuja kumzika bwana wake kwani alikua na hali mbaya kupita maelezo ,alikua amevunjika vunjika miguu yote ,mikono pamoja na mshipa wa uti wa mgongo ulicheza ,,madaktari walikua wakifika kitandani alipo na kutimiza tu majukumu ila walijua wazi huyu hamalizi hata wiki
Kweli kama madaktari walivyosema madaktari ,baada tu ya mazishi ya baba kenedy ,mama kenedy na yeye aliaga dunia,kilio kilitanda kwa ndugu jamaa na marafiki ,ila kila mmoja alielewa wazi yaliowakuta hawa niroho mbaya mzee mmoja alisema
``kuna saa hadiMungu anashindwa kuvumilia masi wafanyayo wanadamu kwa kweli duuuh yaan hawakupata hata wakujutia kifo kiliwachota fastaaa duuuh Mungu tupe mwisho mwema ,,’’
Baada ya wiki moja kupita hali ya jesca iliendelea kuimarika jesca alinawiri ,tabasamu lake lilichomoza tena ,dokta Hussein alifurahi sana hali ya jesca ilivyokuwa ,nesi subira nae alifurahishwa sana na kupona kwa jesca ,walimpongeza sana ,mtihani ulitokea hapa
Je mgonjwa kapona ,sasa apelekwe kwa nani

Siku  moja dokta Hussein akiwa kazini kwa mbali alimwona jesca akija kwenye ofisi yake
Jesca alipofika mlangoni alibisha hodi ,dokta alimruhusu kuingia ,jesca kwa uchungu sana alimshukuru Hussein hakuwa na lugha ya kutamka juu ya upendo mwingi aliofanyiwa jesca alijikuta akisema
``Mungu akubariki sana kaka natamani ata ningeendelea kuishi hapa nikuone wewe ,umekua ,mwema kwangu sijawahi ona’’
Hussein alimshukuru sana jesca ,Hussein muda wote jesca akiwa anaongea alimtazama tu usoni alijikuta akivutiwa sana na yule binti Hussein alitamani amweleze jesca kilichoujaza moyom
Jesca nae alihisi kitu kwa mshangao aliuliza
``kaka husssein mbona waduwaa’’
Hussein alivunja ukimya alimweleza kila kitu jesca alimwambia jesca ikiwezekana wakaishi wote ,Hussein alimweleza jesca historia yote na kila kitu kuhusu maisha yake
Jesca alijikuta akikubali kwani aliyofanyiwa na dokta ni mengi mno hakuwa na cha kulipa
Hussein alifurahi mno kukubaliwa ombi lake na jesca alimshika jesca na kumkumbatia kwa furaha ,wakiwa wanakumbatiana ghafla nesi subira aliingia
Jesca alimsalimu kwa furaha hali kadhalika Hussein alimsalimu
Cha kushangaza subira hakujibu alitupa faili kwenye meza ya Hussein kisha alitoka nje
Subira alipitiliza hadi nje chini ya mti wa kivuli aliuma mdomo kwa hasira
``huyu dokta Hussein kumbe kumtunza huyu binti na kumtibu kote kumbe alikua akimtaka kimapenzi ,,,Mungu wangu sasa mimi kila siku namendea nyuma ni kuwa dokta anipendi au daaah huyu mporipori asiye na kwao anapendwa na dokta haaaa’
Subira alichukia sana aliingia maabara na kuchukua sindano yenye sumu alipanga kuwa ikifika muda wa kumchoma jesca sindano ya kukausha vidonda lazima amchome sindano yenye sumu ili amuue kabisa asije mwachia nafasi ya kumchukua Hussein
Ilipofika saa mbili usiku ,jesca akiwa kitandani huku akiwa na furaha tele ,aliwaza sana juu ya maisha yake ,hakuamini kama atakuwa mke wa dokta alimsukuru Mungu sana aliamini ,maneno ya Mungu kuwa ``mungu anaweza kumtoa mtu mavumbini na kumketisha palipotukuka
Akiwa anawaza hivyo ,nesi subira aliingia akiwa ameshikilia vifaa vyake vya kazi ,sindano na dawa …
Je jesca atapona ,,,,mkasa huu umejaa visa vingi vya kusisimua na kufundisha endelea kufuatilia
Share sasa tuendelee ,like ,comment


No comments

Theme images by jangeltun. Powered by Blogger.