NZIGE WAFIKA SUDAN
Mlipuko wa nzige mbaya kabisa kutokea Afrika Mashariki katika miaka 70 umefikia Sudani Kusini, nchi ambayo karibu nusu ya idadi ya watu tayari wanakabiliwa na njaa baada ya miaka ya vita vya wenyewe kwa wenyewe, mamlaka zimesema.
Waziri wa Kilimo Onyoti Adigo aliwaambia waandishi wa habari kuwa kundi la nzige lilionekana ndani ya nchi, lakini amesema pia mamlaka itajaribu kudhibiti mlipuko huo.
Nzige wameonekana katika jimbo la Equatoria Mashariki karibu na mipaka na Ethiopia, Kenya na Uganda, nchi ambazo pia zimeathiriwa na mlipuko huo ambao umesababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa.
No comments