NDEGE ILIYOPOTEA NA KUREJEA DUNIANI BAADA YA MIAKA 37


Ndege aina ya PAN AMERICAN FLIGHT namba 914 iliyokuwa ndege ya kimarekani ilikuwa ikitokea Newyork kuelekea Miami tarehe 22 julai 1955

Ndege ilipaswa kuingia Miami saa 9 na dakika 55 julai 1955 kutokea newyork cha ajabu ndege hiyo ilipitiliza kilomita takriban 2000 kutoka mahali pale ilipotakiwa kutua na ikabaki ikizurula tu angani. Huku marubani wakiwa hawajui nini cha kufanya ndege hiyo ilipotea katika rada na hivyo hawakujua wapi ilipo na mawasiliano yalipotea kabisa.

Ndege hiyo ikiwa katika anga iliendelea kuambaa ambaa huku na kule kwa sababu ilikosa udhibiti kutoka kwa muongozaji. Baada ya muda ndege hiyo ilipotea kabisa haikuonekana tena na haikujulikana wapi imeenda au ilipotelea wapi.

Juhudi kubwa za kuitafuta zilifanywa bila mafanikio yoyote  utaalamu wote uligonga mwamba na hivyo maisha yaliendelea tu

Sasa basi jambo la kushtua lilijitokeza baada ya miaka 37  ndege hiyo ilirejea duniani tena mnamo septemba 9 mwaka 1992 katika uwanja wa ndege wa Venezuela. Jambo kubwa sana ni kwamba ndege ile ilirudi ikiwa vile vile na watu wale wale haikubadilika chochote watu hawakuzeeka au sura zao kubadilika bali walirudi kama walivyopotea


Maswali ya kujiuliza

Je nini kilitokea katika ndege ile?
Je ndege ile kwa miaka yote 37 ilikuwa ikitumia mafuta kutoka wapi?
Je abiria walikuwa wanakula nini?

Usiache kuweka maoni yako hapo chini.

No comments

Theme images by jangeltun. Powered by Blogger.