KAULI ZA JPM
Watanzania mlinichagua kwaajili ya kuja kusimamia haki na utendaji ndani ya serikali ili kila fedha inayochangwa itumike kwa mujibu wa sheria na ndio maana mtaona miradi hii inatokea ni kwasababu tumebana na tunataka miradi yote iende kwa mujibu ilivyopangwa kwahiyo saa nyingine msisikitike sana mkimuona mnamuonea huruma ili kusudi akajifunze vizuri huo ndio ukweli na siku zote nitasimamia ukweli,” – JPM
Hivi karibuni palikuwa na mkataba wa ajabu unatengenezwa Wizara ya Mambo ya Ndani wenye dhamani wa Euro milioni 408 na mradi huo umetayarishwa na kusainiwa na Kamishna Jerenali wa fire haujapangwa kwenye bajeti wala kupitishwa na bunge, wakati wa vikao na kampuni moja nafikiri kutoka Romania wahusika wote wa watanzania waliokuwa wanakwenda kwenye majadiliano wanalipwa ‘sitting allowance’ ya Dola 800 bado ya kulipiwa kwenye tiketi za ndege wakausaini mradi wa hovyo lakini masharti yanasema ukitaka kuuvunja yale ambayo yameshaanza kutekelezwa lazima yaendee kutekelezwa,” – JPM
Ninashangaa kuwaona Kangi Lugola na Kamishana Jenerali bado mko hapa sitaki kuwa mnafiki mtu anasaini zaidi ya Sh trilioni moja wakati sheria zote zinajulikana mwenye mamlaka ya kukopa fedha kwaajili ya Tanzania ni Wizara ya Fedha peke yake ikiwa hivyo kila mtu atakuwa anakopa hata mimi nitakopa sasa mimi nitaendelea kuwapenda lakini kwenye position hii no,” – JPM
Mimi ninampenda sana Kangi Lugola ni mwanafunzi wangu nimemfundisha pamoja na mwili wake na ukubwa wake lakini kwenye hili hapana nilitegemea hata hapa nisingemkuta hatuwezi kuendesha nchi kwa misingi ya ajabu namna hii yanayokwenda kununuliwa kule kwenye mkataba ni ya ajabu mno,” – JPM
No comments