BINADAMU ALIYESHIKA REKODI YA KUWA NA TATOO NYINGI MWILINI

Lucky Diamond Rich, ndiye mtu mwenye tattoo nyingi mwilini kwa rekodi ya mwaka 2019


alizaliwa New Zealand, akiwa anaitwa Gregory Paul McLaren,

"Diamond limekuja kuwa jina langu kwa kuwa marafiki zangu wananiita Almasi chafu, na pia wameniita Rich(Tajiri) kwa kuwa mimi ni tajiri wa kiroho"

Rekodi ya kuwa na tatuu nyingi ameishikilia kwa Zaidi ya muhongo,

Huyu bwana hutumia muda mwingi kuboresha tattoo za mwili wake

Mbali na tatuu alizonazo, huyu ndugu ametoboa masikio na kuyavuta(kama wamasaii), na meno yake ameweka mawe ya madini ya fedha(silver), pia amejitoa sehemu kadhaa za mwili wake

Alianza kujiweka michoro mwilini mwake akiwa na umri wa miaka 16, kwa kuwa kazi yake ni maonyesho aliendelea kujichora hadi akawa mtu anayeshilia rekodi ya kuwa na michoro mingi

Alimaliza kujichora mwili wake akiwa na umri wa miaka 28 na akaanza kuziboresha michoro aliyo nayo


"Hapana. Sijutii lolote nililonalo au nililofanya. Nadhani huo ni woga ambao watu wengi wasio na michoro mwilini.Michoro ya mwilini unaweza ukaitengeneza uwezavyo, ukaifunika, ukaibadilisha au ukaifuta."

Lucky hajajiweka michoro mipya kwa takribani miaka 6 na bado hakuna aliyekuja kuvunja rekodi yake

No comments

Theme images by jangeltun. Powered by Blogger.