KUSUKUMWA NA UPENDO 2
Hadithi=> KUSUKUMWA NA UPENDO
Sehemu ya : 2 ***msituni
“Lakini Bruchko”, Bobby akasema, “hakuna usalama kweli katika mambo haya, Mungu tu anaweza kutusaidia.” Sisi watatu tuliinamisha vichwa vyetu na kuzungumza na Mungu pamoja. Wakati tulipoomba, hofu yangu ilitoka. Ilibadilishwa na furaha ile ile ambayo ilinijia wakati nilipomwona Bobby asubuhi siku ile. Furaha ile iliingia moyoni mwangu, hata tumboni mwangu. Lakini haikuwa furaha ile ile. Ilikuwa ni furaha yenye nguvu zaidi kama vile huzuni, hatari na hofu zilivyokuwa zimeingia ndani yangu.
Mambo mengi yalikuwa yametokea kwa masaa machache tangu ndege yangu ilipozunguka juu ya mji wa Rio de oro kabla yakutua. Kwa mbali chini yangu niliweza kuona msitu mpaka upeo wa macho kama zulia nene la kijani. Upande wa kulia nilianza kuona kama ufuo wa rangi ya kunde. Ulikuwa ni mto wa Catatumbo. Tulipopita niliona mkusanyiko wa nyumba za mji ule. Karibu zote zilikuwa mpya. Mji ulionekana kama mpotevu ndani ya msitu.
Lakini mji unakua, nilifikiri. Wazo lilinijia ya kwamba miaka kumi iliyopita hakukuwa na kitu chochote mahali pale isipokuwa miti mirefu ambayo ilizuia nuru ya jua kufika chini, na majani mengi chini ya miti. Labda mtu angeweza kuwasikia kasuku wakilia wakati ule. Lakini sasa mahali pale palikuwa na mji.
Niliingiwa na furaha, si kwa sababu ya mji ule, lakini kwa sababu nimerudi kutoka Amerika na kwa sababu baada ya muda kitambo nitaunganishwa tena na Bobby, ndugu yangu ambaye nilifanya mapatano naye. Nilifungua dirisha ili kujaribu kuona mbele kidogo na nilijaa matumaini makubwa sana.
Wakati ndege ile DC 3 ya zamani ilipokuwa ikikaribia kutua, miti ilikuwa karibu sana kiasi kwamba ilionekana kwamba labda magurudumu ya ndege yatashikwa na miti kasha tungeanguka. Lakini ghafla tulitua juu ya kiwanja kirefu chembamba katikati yam situ. Tulitua chini a breki zilivutwa kwa nguvu kusimamisha ndege juu ya kiwanja.
Tulipofika mwisho wa kiwanja cha ndege nilitazama ili nimwone Bobby kati ya watu, sikumwona. Lakini tuliposhuka niliweza kumwona pembeni kidogo, mfupi mwenye mwili wenye nguvu akiwa amevaa shati nyekundu na suruali nyeusi. Uso wake ulikuwa na rangi ya kunde zaidi kuliko wengine waliokuwa wakisubiri mahali pale. Kwa mbali niliweza kuona jinsi meno yake meupe yalivyong’aa. Ilikuwa ni tabasamu yenye kumaanisha: “umerudi tena Bruchko, ni vizuri.” Hakutumia kamwe jina langu la kiamerika, Bruce.
Nilianza kukimbia. Nilipomfikia nilimshika na kumsalimu salamu ya kimotilone. Nafahamu ya kwamba waliotuona walishangaa. Mhindi mwekundu mfupi mweusi aliyemkumbatia Mmarekani mrefu mweupe. Lakini kwetu sisi haikuwa kitu.
“Ndugu yangu”, nilisema, “ndugu yangu Bobarishora”. Nilimwita kwa jina lake la nyumbani kama nilivyozoea kumwita kwa wakati maalumu. Nilirudi nyuma hatua moja. Kisha nilimwambia: “Unaonekana u mzima. Mke wako yu hali gani? Na mtoto mvulana hajambo?” “Ndio mke wangu yu mzima”, Bobby akasema. Ana afya nzuri na yu heri. Na anafurahi kabisa kuwa mama wa motto mvulana na mwenye afya pia. Kwa hiyo nafahamu motto yu mzima. Ndio yu mnene sana. Ungemwona! Na ameanza kuzunguka zunguka nyumbani kama nyani mdogo.
“Njoo”, aliendelea kusema, “afadhali tusikae hapa siku nzima. Twende tupokee mizigo yako.” Tuliporudi kwenye ndege ambapo mizigo yote ilidaiwa, Bobby aliuliza, “Na shughuli zako zote huko Amerika, je”? Nilikumbushwa juu ya watu wote wa vyumba vyote vyenye kufanana.
“Sijui Bobby. Nafikiri nimemaliza shughuli zote ambazo nilipanga kwamba nitazimaliza. Lakini nafurahi sana kurudi tena hapa”!
Bobby aliongea habari za jamaa yake. Alikuwa na furaha ile ile ya zamani. Macho yake meusi yaling’aa. Nilihuzunika kwa ajili yake niliposikia ya kwamba binti yake amefariki. Kwa majuma kadhaa alikuwa mwenye moyo mzito kwa sababu ya huzuni. Wakati huu alikuwa hawezi kujizuia kutabasamu.
Baada ya kupokea mizigo tulikata shauri kula chakula. Tulikwenda mjini karibu ya kiwanja. Barabara nyembamba za changarawe zilijuaa nyumba mpya, paa zake za bati ziling’aa kati ya kuta za zamani zisizopakwa rangi, za majani ya michikichi. Nyumba zilionekana zimetuna kama kwamba haziwezi kudumu kwa muda mrefu.
Sikupata chakula kwenye ndege na Bobby alinicheka jinsi nilivyojishibisha na chakula cha Colombia.
“Tangu sasa utakuwa na tumbo lililojaa Bruchko”, akasema. Nilifahamu alikuwa na maana gani. Kwa mmotilone kuwa na tumbo lililojaa ilikuwa si maana tu ya kwamba chakula kinamtosha. Maana yake ni hali ya utulivu, satarehe na maisha ya uheri. Alieleza sawasawa na hisia zangu.
____ITAENDELEA____
usikose kufuatilia pia toa maoni yako
No comments