NAJUTA KUZALIWA MWANAMKE 09


ILIPOISHIA…………………………………………..
Taratibu za mazishi ziliendelea ,msiba wa Hussein ulikua ni pigo kubwa sana ,,,ilipofika siku ya mazishi  ,,watu walifurika jesca alilia sana ,ndugu jamaa na marafiki walilia sana
Wakati wa wosia wa marehemu  kusomwa watu walitulia kimya kusikiliza ,kilichowashangaza watu pamoja na jesca ni hiki
Iliposomwa wosia waliandika ``Marehemu amefariki akiwa hana mtoto wala mke’’
Jesca alihisi kuchanganyikiwa alijisemea ``mhhh itakuwaje kwa hiyo mimi siyo mke wa hussein’’
Jesca aliamua kupotezea ,pole zilitolewa ,watu walimruka jesca hakuna aliyemjali jesca kama mfiwa ,,,jesca alimuuliza wifi yake ajulikanae kama cathe
``wifi angu mbona mimi sitambuliki kama mke jamani  au kuna kitu gani jamani nijue’’
```mhhhh pole mama ndio wameamua hivyo sina la kukusaidi’’
Baada ya msiba kuisha kila ,,habari za Hussein zilisahaulika
Kutokana na hussein kuwa na hela nyingi ,majumba na magari pale mjini ,ndugu zake waliamia mjini ,ikiwa ni pamoja na mama baba na cathe dada wa Hussein
Siku moja asubuhi kama ilivyokuwa kawaida ,jesca mke wa marehemu aliamka na kwenda sebuleni
Aliichukua picha ya Hussein na kuibusu huku akitamka
``mume wangu mpendwa naamini ulipo upo mahali salama ,naahidi kutunza na kukileta kichanga duniani ,kama ulivyoniambia huyu ataitwa happy ,furaha ya ulimwengu ,hivyo na kuahidi kutimiza ‘’
Jesca akiwa anasema hayo mama mkwe  wake alikua nje kidogo alisikia yote ,kwa haraka alifunga kanga yake vyema nakuingia sebuleni
``wewe kahaba funga bakuli lako ,mchawi mkubwa wewe ,unasema unamimba ya mwanangu ,Malaya wewe uliyeokotwa sijui hata kijana wangu alikupendea nini wewe kisura chako cha kikahaba kabisa ‘’
Maneno yale yalizama kama msumari wa moto moyoni mwa jesca ,jesca alihisi kuishiwa nguvu ,,,,,picha ya Hussein ilimchomoka na kudondoka chini
Mama mkwe aliendelea kuropoka
``kahaba wewe unaona hadi picha ya mwanangu ina kukimbia hahahah nikifumba macho na kufumbua ……’’ kabla hajamaliza kusema baba mkwe wa jesca aliingia na cathe ‘’
Mama Hussein alibadili mada kidogo na kusema
``nilikua na mwambia huyu ajitahidi kujituma maana kila mara yeye ni wa huzuni tu toka msiba uishe utendaji wake ni mdogo ,usafi anafanya kwa kujifuta sijui kama na nyie mmeliona  hili jamani’’
Cathe alimsogelea wifi yake na kumshika kisa aliaanza kumbembeleza
``wifi usilie jamani yale yameshapita sisi wenyewe tunampenda Hussein siyo kuwa tumeshindwa kulia laaa sisi  tunasikilizia maumivu kutoka ndani ,maskini kaka angu alikua mtu bora sana kwangu hata kunisomesha ni yeye alifanya hivi nampenda sana ningeweza lia mwaka mie ila ni kuwa najikaza ‘’
Laity kama cathe angejua kwanini jesca analia ,jesca alikua analia sababu ya maneno ambayo mama mkwe wake amemtamkia ,mama ake na Hussein alikua ni mwanamke katili na mnyama sana ,huo mdomo wake si wan chi akianza kuchamba watu kila mtu alikua akipiga kimya maana ukiingilia na wewe unapata dongo kubwa
Wote walitawanyika na kila mmoja aliendelea na kazi zake
Jesca alianza kazi ila moyo wake ulikua ukivuja machozi ,moyo uliuma sana  alijisemea
``kweli mama mkwe unaniita mimi ni kahaba ,,mama mkwe una niita mimi mchawi .,,,Mungu wangu nimekukosea nini mja wako nisie na kwetu nateseka kama mnyama mimi ‘’
Wakiwa wanaendelea na kazi  walisikia hodi katika familia ile ,,,,,,
``Hodi hodi’’
``karibu karibu ‘’ cathe alienda kufungua ili waweze kuingia
Walikuwa ni wafanyakazi wenza wa Hussein ,walikua bado hawajatoa salamu zao za rambirambi ,hivyo walikuwa wametuymwa wawakilishi wachache ,cha kushangaza siku hiyo na nesi subira aliyekuwa anataka kumuua jesca alikuwepo ,,,,kumbe baada ya Hussein kufa nesi subira aliachiwa mahakamani kwani mahakimu wengi wanapenda kitu kidogo ,wazazi wa subira walikua ni matajiri sana ,walitoa hela ndefu sana ,subira alitolewa mahakamani na kazini alirudi
Shoga zake na subira walianza kumpongeza
``hahahah subira mama wewe ni noma ,usikute wewe mchawi yaan Hussein anakupeleka jela kwa kutaka kumuua mke wake ,na Hussein anakufa kabla hata ya wiki kuisha ,kweli wewe mchawi mama’’
Subira alicheka kwakebehi ``haahahahaha huhuhuhuhu ukitaka kupambana na mwamba utaumia mwenyewe’’
Wageni wale walikaribishwa vyema ndani ya nyumba ile ,,baba Hussein na mama Hussein waliwapa heshima kubwa kwani walijuwa kuwa hawa ni madaktari wenza ,na waliamini kuwa watashirikiana nao kikamilifu
Subira pamoja na madaktari walikaa pale ,kabla ya yote subira alisema
``vipi jamani mke wa marehemu yuko wapi’’
Subira aliuliza kwa kinafiki
Jesca aliitwa ili aweze kupewa pole
Jesca alipoingia sebuleni hakuamini kumwona subira alidhani anaota ,kwani subira ilisemekana baada ya kutaka kufanya mauaji alifungwa kifungo cha maisha sasa inakuaje leo na kazini yupo
Subira alijua jesca anachowaza mbele ya watu wote alicheka
``jesca upo mama mke wa marehemu Hussein huhuhu’’ subira alisalimia kwa kejeli sana
Jesca alijua hapa anafanyiwa masihara alitoka nje kwa hasira ,,subira kwanza alitaka kumuua leo iweje yeye anaeleta rambirambi jesca aliingia ndani ya chumba alichokua akikaa na hussein kisha alijifungia
Kitendo hiki kiliwachafua watu sana si mama si madaktari si wifi si baba mkwe
Mama mkwe alianza kuropoka
``unaona huyu mbuzi alivyo na kiburi ,sasa huyu nasema hastahili kukaa hapa ‘’
Subira alidakia
``yuaaan nyie wazazi wapumbavu hata hamkujiuliza ,inakuaje mtu anaoa mke hamalizi hata siku tatu yeye anakufa ,huyu mwanamke wenda hata si binadamu wa kawaida ,,mmekaribisha laana katika familia ,huu ni mzimu usio na kwao ,mimi mwenyewe nilijaribu kumshauri marehemu siku za uhai wake aachane na jesca ila nilichoambulia ni yeye kunitengezea kesi ya kutaka kuuwa ,leo na tamka mbele yenu  mimi sikuwa na lengo hilo ndio maana mnaniona nikiwa hapa leo ,ila simlaumu mtoto wenu ,na mlaumu huyu takataka mwanamke asiye na kwo jesca ,hakika huyu ndio shetani tena ndio kamloga mume wake huyu ,,Hussein dereva mzuri ameendesha gari miaka nenda miaka rudi ,huyu kikaragosi analetaje shida khaaaa fukuzeni ‘’
Mama mkwe alihisi kuchanganyikiwa hadi baba mkwe alilogeka walihisi anayoyasema subira ni kweli
Kwa jinsi  mama mkwe alivyokuwa akimchukia jesca alinyanyuka akisema
``wewe kahaba chukua kila kilicho chako usizidishe chochote nakupa nusu saa uende kiwenu wewe ,mchawi mkubwa wewe,tena wewe ni mzimu usio na kwao’’
Jesca akiwa chumbani alisikia yote
Alijua hali imeharibika taratibu ,alinyanyuka hakuwa na kipingamizi alitoka nje na kuwafuata
Alipiga magoti na kusema
``jamani nisameheni nimekosea  ila mngejua uchungu nilio nao mimi msingesema yote haya ‘’
Mama mkwe aliropoka
``kama una uchungu zaa mbwaa wewe ,,,,,si umesema wewe una mimba ya Hussein ,sasa unamimba hujawahi tapika ‘’
Wote walicheka kwa nguvu si madaktari si baba ,subira ndio alicheka kabisaaa ,ila cathe alikua akimpenda sana jesca hivyo alisononeka tu hakuwa na namna
Jesca alifuatwa na mama mkwe
``nimekupa nusu saa ,sasa ikipita nitakutoa kama mwizi jiandae mwenyewe ‘’
Jesca aliona hana namna ya kulazimisha aliingia ndani alichukua kila kilicho chake kisha alichukua picha moja ya Hussein na kuificha ndani ya kimfuko kidogo
Alipomaliza aliwafuata na kuwaaga
Mama mkwe aliropoka
``hebu ngoja nimkague huyu nasema ,huyu ni mwizi lazima tumshike na kitu cha wizi ‘’
Mama mkwe alimwaga vitu vyote chini alipekua kwa bahati mbaya picha ya Hussein ilionekana
Mama mkwe aliinyanyua na kusema
``hahah mnaona nilichowaambia huyu mwizi huyu picha anapeleka wapi ,kahaba wewe lete picha sepa na mia’’
Jesca alinyang’anywa kila kitu alibakiziwa vinguo viwili vitatu alivyonunuliwa na mumewe
Jesca alichukua mfuko wake na kuanza kuondoka
Akiwa anaondoka ,cathe aliingia chumbani kwa haraka alipiga mkono kwenye begi lake alitoa picha moja ambayo walipiga siku ya sherehe ilikua ni picha ya Hussein akiwa jesca pia alitoa picha moja akiwa Hussein peke yake
Cathe alimkimbilia jesca kwa bahati nzuri alimwona kwa mbali aliita
``jescaaaaaa’’
Jesca alisubiri
Cathe alianza  ``wifi nisamehe tambua mimi siko upande wa hawa jamani nakupenda sama ila sina namna ya kukusaidia my dia ,nimekuletea hizi picha zitakuwa kama kumbukumbu  kwako’’
Jesca alipokea picha zile alipotazama picha aliyopiga na hussein machozi yalimtoka upya
Jesca alimshukuru sana cathe na kumwahidi kuwa ipo siku
Cathe alimpatia jesca shilingi elfu tano na kumwambia
``wifi sina chochote ila hii itaweza kukufaa japo hata chai’’
Jesca alimkumbatia wifi ake kisha waliagana
Cathe alisikia uchungu sana ila hakuwa na namna
Jesca alianza kukata mtaa asijuwe wapi wanaenda
Akiwa anatembea kwa mbali aliona gari jeusi ,moyo wake uloigonga
``Paaaaaaa’’ kwani gari lile limefanana kabisa na gari la mama chuchu aliyemteka kipindi kile
Jesca akiwa anashangaa taratibu gari lilisogea karibu kabisa na yeye kama vile linamfuatilia


Je nini kitaendelea ………………………………………………………………………………………………………………………
Mkasa huu utaendelea share like na comments

No comments

Theme images by jangeltun. Powered by Blogger.