GM NA HONDA WAMEZINDUA GARI LINALOJIENDESHA LENYEWE
GM na HONDA wenye uzoefu kwa zaidi yq miaka 160 wamezindua gari mpya inayojiendesha yenyewe
Gari ya umeme yenye viti sita haina usukani wala breki wala kiongeza mwendo hakuna wipers wala side mirror. Gari hiyo haina mbele wala nyuma kama gari za kawaida
Mwanzoni wateja hawataweza kununua gari hiyo lakini wataweza kupanda moja kwa moja kupitia program maalum
Ka kawaida gari hii imefungwa sensor maalumu kwa ajili ya ugunduzi wa uzito na kigundua ikiwa abiria kafunga mkanda na pia kubaini ikiwa abiria ameingia au ameondoka kwenye gari
Watendaji wa gari hiyo walisema kuliondoa gari hilo katika sifa ya gari za kawaida kunaruhusu nafasi zaidi kwa abiria kwani mlango wa kuingilia ni mpana zaidi kuliko gari za kawaida, wakati huo ina uwezo wa kuruhusu watu wawili kuingia na kutoka kwa wakati mmoja.
Gari hiyo imeundwa kwa ajili ya kutembea barabara zote za jiji na barabara kuu.
Kampuni hizo pia hazijaweka bayana ni lini zitaanza uzalishaji wa gari hiyo au ni lini itaonekana barabarani lakini walisema haitachukua muda hivi karibuni tu.
Taarifa zaidi kaa ukifatilia makala zaidi kutoka kwetu @the master pizo
No comments