KUSUKUMWA NA UPENDO 4




Hadithi=> KUSUKUMWA NA UPENDO
Sehemu ya : 4 ***msituni
 Nilimtazama Bobby aliyekuwa ameshika usukani wa mashua nikatabasamu. Ilikuwa ajabu tya kwamba nilifika mahali pale tena na kwamba nilikuwa na ushirika na watu wale. Ilikuwa ni Mungu aliyenipeleka kule. Nisingeweza kufika kule mimi mwenyewe. Na kama ningependa kufika huko nisingeyashinda matatizo na hatari zote peke yangu. Kweli nisingeacha nyumba yangu huko Minneapolis, kama nisingekuwa na Mungu ndani yangu, yeye aliye na nguvu.
 Nilipokuwa nimeketi ndani ya mashua, nilimssukuru Mungu kwa ajili ya Bobby, kwa ajili ya Wamotilone, kwa ajili ya msitu ambao ulituzunguka pande zote na hata juu yetu kama hema. Miti mikubwa yenye matawi membamba marefu, ilikuwa imenyooka kuelekea juu ili kupata mwanga. Mwanga wa jua haukuweza kufika hadi ardhini kwa sababu ya msongamano wa miti.
 Majani madogo madogo mengi yalining’inia kila upande wa mti. Na chini yake kulikuwa na mimea mbali mbali, ya kijani kibichi yenye kupendeza.
 Mto ulipokuwa mwembamba, tulisafiri chini ya miti. Ilionekana ni giza kama usiku. Hli ya hewa ilikuwa yenye joto na unyevunyevu. Aina ya wadudu jamii ya kunguni walituzunguka na kutuuma.
 Lkini nilikuwa na furaha mno. Mahali pale palikuwa ni nyumbani kwangu. Mahali pengine pote nilijisikia mgeni. Tuliendelea na safari yetu kwa muda wa masaa matano na nusu. Hakuna hata mmoja kati yetu aliyejaribu kuzungumza. Hata hivyo tulikuwa na mawasiliano. Wakati mwingine tulionyeshana na kukumbushana juu ya mambo mbalimbali tuliyojionea. Hatukuona uhai mtoni. Kwa muda mfupi  tu tuliweza kuona ndege kwenye miti kasha walitoweka.
 Tuliposimamisha mashine yetu ili kuweka mafuta , tuliweza kusikia milio ya wanyama. Lakini hakukuwa na makao ya watu wanaoishi sehemu ile.
 Kwa ghafla tulitambua kutoka mtoni kwamba tulikuwa tumekaribia mji akiishi Ayaboquina.
 Bobby alinitazama mwenye uso wenye swali, akionyesha kwa kidole upande wa nyumba zilizokuwa juu ya jabali. “Je, unataka kusimama”? aliuliza. Niliinamisha kichwa kuonyesha kwamba nimekubali. Aliendelea hadi ukingoni.
 Tuliufunga mtumbwi kwenye mti kasha tukapanda lile jabali kwa haraka. Pale juu karibu na nyumba tuliona alama kubwa mpya. Alama ile iliandikwa kwa herufi kubwa ikieleza kwamba “Mbele ni nchi ya wamotilone na kwamba hairuhusiwi kuishi kule.”
 Nilionyesha kwa kidole kwenye ule ubao. “Je, serikali imeweka tangazo hilo na uamuzi huo?”
 “Ndio, majuma mawili yaliyopita.”
 Tuliuliza ikiwa tunaweza kumpata Ayaboquina. Mmoja wa wanawake alituambia kwamba alikuwa karibu na sehemu iliyofyekwa. Walikuwa wakijenga nyumba mpya, na vile vile sehemu ile wangejenga shule na kituo cha afya.
 Ilikuwa ni mahali palke tulipokutana na Ayaboquina na kutishwa na Humberto Abril.
 Baadaye niliyakumbuka yale maneno, “kwa msalaba huu nitawaua.” Maneno yale yalikuwa ya baridi – yasiyofurahisha. Je, yalikuwa matusi tu, vitisho tu? au yalikuwa na maana? Je, yalikuwa ni maneno yenye kutabiri kitu ambacho msalaba ungeleta kwetu?
 Ilikuwa ni kwa ajili ya msalaba niliweza kuwapenda Wamotilone na wao kunipenda mimi.
 Lakini je, ningekufa kwa ajili ya msalaba pia? Je, Bobby pia ungekufa kwa ajili ya msalaba?
____ITAENDELEA____

No comments

Theme images by jangeltun. Powered by Blogger.