NAJUTA KUZALIWA MWANAMKE 18


NAJUTA KUZALIWA MWANAMKE 18
Akiwa anawaza vile wazo chafu lilimjia mama mkwe alijisemea
``hivi manesi nikiwapa kitu kidogo waue hiki kichanga si dakika mbili tu ,waulie mbali kwanza huyu  mtoto haijulikani hata baba ni nani’’
Akiwa anawaza hayo nesi secy alipita
``samahani dada ‘’
`bila samahani’’
``ok nitakupa chochote utakacho waweza kukiua kichanga cha huyu binti ‘’
`kwanini mama kuna tatizo ‘’
``ndio mtoto anaugomvi wa kifamilia ‘’
``ok mama njoo pembeni’’
Secy alimnong’onezea mama mkwe
``shilingi laki tatu ‘’
Mama mkwe alipiga mkono kwenye begi kisha alitoa nusu ya hela ile  yaan laki moja na nusu
Kisha alimpa nesi secy ,secy alifurahi alimwambia
``si mtoto tu afe au niue na mama ake ‘’
``ungeweza hata wote ni sawa mwanangu’’
Nesi secy alirudi wodini kwa haraka
``je nini kitaendelea ………………………………………
Nesi secy alipofika wodini alimtazama jesca aliyekuwa kilia kwa uchungu kwani mtoto ndio alikua ashaanza kutoka ,,,,,manesi walisogea karibu ili kumzalisha jesca
Ndani ya dakika kumi na tano kichanga kilitoka salama kabisa alikua ni mtoto wa kike kama Hussein alivyomwambia mkewe ,ila hali ya mama mtoto haikuwa njema kabisaa jesca hakusaidiwa vyema katika suala zima la kuzalishwa hivyo damu nyingi zilimtoka hii ilimpelekea kupoteza kabisa hata nguvu mwilini na kushindwa hata kauamka kwa muda ule
Nesi secy alikimbilia kichanga kile ,alijisemea
``Kwa jinsi hali ya mama yake ilivyo mbaya sasa huu ndio wasaa wa kumuua huyu mtoto’’
Nesi secy huku akijificha ficha sana  alikibeba kichanga kile na kukiingiza nyumba ya watoto njiti watoto waliozaliwa kabla ya umri wao ,secy alijisemea
``sasa nikiwa huku haka lazima nikaue kabisa’’
Upande wa pili hali ya jesca iliendelea kuwa mbaya yalipita masaamatano hajazinduka ,alisikika daktari mkuu akisema
``jamani hapa hatuna namna  ya kumsaidia huyu binti ,katika hospitali yetu hamna damu kundi olake tungemwongezea na amebakiza masaa machche afe ‘’
Taarifa zilifikishwa kwa mama mkwe ambaye ndio alikua pale hospitali ,daktari alimfuata na kumwambia
``mama binti yako katika kujifungua ametoa damu nyingi hivyo anapaswa kuongezewa na kundi lake ni O pambana kabla ya saa tisa aje mtu
Mama mkwe aliitikia ```jamani dokta mbaya sana hii tutafanyaje ‘’
``ok kama upo sawa tukupime wenda ukawa kundi moja umsaidie \\
``akuuuu siwezi’’
Upande wa pili nesi secy aligundua kitu
``kwanini huyu mtoto nisimchukue na kumpeleka maabara ya chini’’
Maabara ya chini ni sehemu moja katik a serena hotel ambamo watoto wachanga mimba zilizotolewa hutupwa huko
Ndani ya maabara ya chini kulikua na harufu ya mizoga ya watu na vichanga hakika hilo eneo ungeliona ungeweza sema ni jehanamu ndogo kwani kulikua na mambo machafu sana
secy alichukua kichanga kile ambacho kilikua kikilia kwa uchungu kwani toka kizaliwe masaa zaidi ya  20 hakijanyonya ,nesi secy alishuka chini kabisa bonde la maabara ,alipoona vichanga na mimba nyingi zilizotolewa taratibu alijkuta akishawishiwa kumuua mtoto ,akitazama mfukoni kibunda cha fedha alizopewa na mama mkwe wajesca zipo na nyingine atapewa baada ya kazi
ilipofika saa moja usiku lilikua limebaki lisaa limoja jesca afe kwani mwili wake haukuwa na damu ya kutosha ,,,mama mkwe alicheka tu
``hahahah nataarifa hii sitoi kwa mtu yoyote wacha huyu nguruwe afe tu tena na kitoto naamini kitakuwa kimeshakufa tayari’’
Kwa muujiza wa ajabu mama mkwe akiwa pale ofisini alishangaa kumwona  cathe mwanae akiingia na chupa ya uji ,cathe alizama moja kwa moja  hadi wodi ile aliyepo wifi ake jesca
Alipofika alishangazwa kuona chumba kipotupu kwa mshangao aliuliza
```yuko wapi wifi yangu jamani ‘’
Daktari alimwambia  ``unamtafuta mgonjwa jesca ,kwa kweli huyu ana lisaa sasa atakufa ‘’
``mhhh shida nini dokta ‘’
``anaupungufu wa damu tumemwambia mama kitambo awaambie hajawaambia ‘’
``duuuh hapana ‘’
Cathe alipima damu kama kundi lake ni sawa na kundi la jesca. Mungu si athumani wa rashidi cathe alikua na kundi O hapo hapo damu ya cathe iliingizwa kwenye mwili wa jesca
Haikupita nusu saa jesca alizinduka huku akisema
``asantee Yesu nimejifungua salama mwanangu,mwanangu yuko wapi’’
Cathe nae alibidi kuuliza mtoto yuko wapi ’’
Madaktari hawakuwa na taarifa yoyote
Upande wa pili nesi secy alishika sindano ya sumu na kutaka kumdunga mtoto shingoni ili afe kabisa ,secy alipomtazama mtoto usoni ,alijikuta akishikwa na huruma ,aliona sura ya rafiki yake wa kipindim kirefu sana ajulikanae kama Hussein aliyesoma nae miaka hiyo
``duuuu jamani huyu mtoto mbona kamfanania Hussein,,,,maskini nimemkumbuka Hussein hivi sasa hivi yuko wapi’’ nesi hakukosea kwani mimba ya  jesca ilikua ya marehemu Hussein
Nesi subira lipomtazama mtoto Yule alichoka ila ghafla alisema
``heri punda afe njiani mzigo ufike ‘’
Alishusha sindano yake hadi shingoni ,alihema kwa nguvu sana kwani alikua maebakiza sekunde chache aue
Jesca upande wa pili alikua akipiga kelele ``mwanangu ,mwanangu ,mwanangu’’
Mama mkwe akiwa nje alijisemea
``huyu nesi mshenzi kweli muda wote hajaua mtoto Yule hadi huyu anazinduka sasa tutafanyaje maana mtoto lazima afe ‘’
Akiwa anawaza hivyo mama mkwe alisikia tetemko alianza kuhisi kizunguzungu
Je ni nini mtoto atapona ,mama mkwe je ,,,jesca je atafanyaje???????????

No comments

Theme images by jangeltun. Powered by Blogger.