NAJUTA KUZALIWA MWANAMKE 15
NAJUTA KUZALIWA MWANAMKE 15
IMETUNGWA NA JOSHUA
Mama mkwe alimwingiza jesca ndani
Ndani ya stoo ile kulikua na vyuma nyaya za umeme
Mama mkwe alianza kusema
``sasa leo ndio utanitambua mimi ni nani ‘’
Jesca alicaharazwa na nyaya za umeme ,alipigwa sana
Alipiga kelele ila mama mkwe aliendelea kumpiga
Jesca kutokana na uchovu na upungufu wa chakula alidondoka chini mama mkwe alishika chuma kubwa akaanza kutoboa toboa tumboni huku akisema
``kahaba wewe unajazwa mimvba huko unasema ni ya mwanangu sasa leo natoboa toboa hadi afe kabisa ,toka lini mwanangu azae na kahaba mshenzi kabisa ,’’
Kelele za jesca zilivuta watu wengi ,majirani na wapitaji baba mkwe hakuweza kuangalia ni nini kwani alikua akimhudumia binti yake cathe aliyepigwa chupa ya uso
Mama mkwe kuona watu wamekusanyika
Alifungua mlango na kutoka mwenyewe
Jesca akiwa chini alikua akipiga kelele huku akilia
``eee mungu nimekukosea nini ,nimekukosea nini mja wako mimi kwanini yanipate haya’’
Mama mkwe wake na jesca alivyofika nje aliwakuta watu wakiwa wana mtazama.
Kwa kiburi na jeuri aliwasemesha
``mmefuata nini hapa niwaulize’’
Huwezi amini kila mmoja aliondoka kwani zilikua nidharau za hali ya juu;;’’
Baba mkwe akiwa anapambana na kumuuguza bintiye aliyepigwa na chupa usoni aliingia ndani kumfuata mkewe
Alipomwona mkewe kwa mshangao alimuuliza
``hivi mke wangu upo na utimamu ????’’
``achana na maisha yangu ‘’
``uliza juu ya hali ya mwanao uliyempiga chupa ya uso ,umemjeruhi sana ‘’
``hahahah pumbavu wakubwa nyie ni bora ningemuua kabisa ,alivyokuwa anaingilia mambo yasiyomuhusu alidhania atapakwa mafuta eee’’
Cathe akiwa nje alisikia alichokuwa akisema mama yake, alihisi kuchanganyikiwa hakuamini kama mama yake ni mnyama namna hiyo’’
Mama mkwe aliingia ndani na kumkuta jesca akiwa amelala chini huku akilia
Alimwambia
``wewe mpuzi nakupa siku mbili za kuishi hapa ukiwa unatafuta pa kwenda sawa ,usije tujazia choo hapa mwanamke kahaba wewe usie na haya’’
Jesca alikua akilia tu muda wote hakuweza hata kumjibu mama mkwe
Mama mkwe kumuona jesca akiwa kimya ,alishikwa na hasira sana kwa haraka alimfuata na kumburuza kama kiroba cha mchele ,tumbo la jesca lilichubuka alisikia maumivu na jinsi alivyomjamzito ilikua ni vibaya sana kwake na hatari pia kwa usalama wa afya yake
Jesca alielekea ndani katika chumba chake ,upande wa pili cathe alijikaza na kuendelea na shughuli ila usoni alijifunga plasta kwani alijeruhiwa vibaya na mama yake
Jioni jesca alipelekewa chakula na wifi yake alishukuru na kula sana alikula zaidi ya sahani mbili ,hadi wifi yake alishangaa ila jesca aliweza kuelewa kuwa wifi yake anamshangaa kwa kile anachofanya jesca alisema taratibu
``wifi mwenzako sijala na siku mbili sasa ‘’
Wifi mtu alitokwa na machozi alilaumu na kusema
``maskini ningejua ningekuletea uji mwepesi ufungue nao tumbo
Ilipofika usiku mama mkwe alioga vyema na kujitupa juu ya sofa alishikilia rimoto na kuangalia zake televisheni bila hata huruma wala habari
Bwana ake alimtazama mkewe na kusema
``mke wangu kwa huu unyama uliofanya leo naomba usikae urudie utakufa hata Hussein alipo hana furaha kwa jinsi unavyomtesa mkewe ‘’
``nyamaza blali fuu ,mbwa wewe kahaba wa kiume kama umempenda huyu kahaba kalale nae mbwa wewe’’
Mama mkwe aliachia matusi kwa mume wake kisha alipitiliza ndani kwenda kulala
Usiku wa manane ulipofika ,hali ya utulivu mkubwa ilitanda katika anga lile ,familia nzima si jesca si wifi si mama wala baba wote walikuwa wamelala fofofo
Mama mkwe akiwa kitandani alisikia tetemeko kubwa sana likitikisa ,katika usingizi alianza kubabaika ,ndoto mbaya zilianza kumvaa ,akiwa usingizini alimwona mtoto wake Hussein akimjia akiwa ameshika kisu kikubwa
Hussein alianza kumsemesha
``mama ,,mama angu nilikupenda ,mama angu nilikujali inakuaje leo unaamua kumtesa na kumnyanyasa kipenzi wa moyo wangu jesca ,mwanamke aliyeubeba ujauzito wangu na amejitahidi kuulinda kwa bidii zote ‘’
Hussein aliendelea kumsogelea mama yake katika ndoto, alishika kisu na kutaka kukizamisha kifuani
Mama mkwe alipiga kelele kubwa
``nakufaaaaaa hussein mwanangu usiniue nisamehe mwanangu ,nisamehe mwanangu ‘’
Baba mkwe wa jesca akiwa kitandani alishtushwa na kelele za mkewe kwani mama mkwe alipiga kelele kubwa pia alikua akihema kwa nguvu sana
Baba mkwe alisema
``nini mke wangu’’
``duuuu mume wangu nitaacha nasema nitaacha’’
Baba mkwe alimshangaa mkewe alivyokuwa akisema hakujua ni nini
Mama mkwe akiwa kitandani anaongea na mume wake alipotazama ukutani alimwona Hussein akija tena akiwa ameshikilia kisu
Mama mkwe alihisi kuchanganyikiwa alipiga kelele kubwa
``baba nisaidie mwanao ananiua Hussein usiniue ,usiniue ,simgusi tena jesca ‘’
Cathe akiwa chumbani alisikia kelele kubwa sana alikuja kutazama
Mama alikua akibabaika kama mtu aliyechanganyikiwa
Upande wa pili jesca akiwa usingizini ndoto nzuri ilimvaa
Aliota yupo chini ya mti wa kivuli ,,,,akiwa amekipakata kichanga chake ,pembeni yake alikuwepo Hussein mume wake ,,akiwa anazishikashika nywele za katoto huku akisema
`mwanangu nakupenda wewe ndio faraja yetu ,,,’’
Hussein alimchukua mtoto akampakata kisha akambusu mtoto pamoja na jesca
Jesca alipopigwa tu busu tu ghafla na yeye alizinduka usingizini
Jesca alitamani hadi kulia alipojitazama aliona machozi yakiwa yamejaa mashavuni akiwa anafikiria juu ya ndoto ile alisikia sauti ya mama mkwe
``Hussein usiniue usiniue mwanangu’’
Mama mkwe alikua akipiga kelele kama mwehu
Je nini kitaendelea………
No comments