NAJUTA KUZALIWA MWANAMKE 12
ILIPOISHIA……………………..
Jesca akiwa anaongea na mama shushu kichefuchefu kilimshika akatapika hapo hapo ,ikumbukwe jesca alikua na ujauzito wa hussein ,kutokana na hali ile hadi kichanga kilichomo tumboni kilichukia
Mama shushu kwa panic aliuliza
``wewe jesca usikute wewe ni mjamzito eee’’
Kwa haraka alichukuliwa na kupelekwa kufanyiwa vipimo
Ndani ya dakika mbili aliyemfanyia vipimo alipeleka majibu kuwa jesca anaujauzito wa miezi miwili na nusu
Mama shushu alihisi kuchanganyikiwa alisikia hasira sana kwa haraka aliagiza jesca apelekwe chumba cha kutolea mimba na mimba ile itolewe
Jesca alisikia yote ,,,jesca alikumbuka sana maneno ya bwana ake Hussein ``mke wangu nitunzie kichanga na pindi akizaliwa mpe jina happy yaan furaha ya ulimwengu ;’’
Jesca alipokumbuka maneno hayo alisema kwa nguvu
``hamwezi kutoa mimba yangu kuliko mnitoe bora mniuwe sipooooo tayari’’
Mama shushu alifikishiwa taarifa hizi ,kwa hasira alikuja akiwa anahema sana ,kila aliyemwona alijua hapa kuna mtu anakufa
Wafanyakazi wa mama shushu walipambana sana kumlaza jesca kwenye kitanda ili atolewa mimba aliyo nayo ,jesca alikua na nguvu za ajabu sana hadi mwenyewe alishangaa zimetoka wapi ,alipambana sana aliweza kuwasukuma wanawake watatu waliokua wakimkamata kumweka juu chakitanda cha mauaji ,nikitanda cha mauaji kwani wanawake wengi waliletwa hapo kwa ajili ya kutoa mimba zao
Wakiwa wanaendelea kulumbana mama shushu aliingia akiwa na jazba sana ,alipofika hakuongea sana ,cha kwanza kabisa alimzaba jesca kofi moja zito lililompelekea kuweweseka ,kwa hasira alisema
``panda juu ya kitanda mbwaa wewe kabla sijakusambaratisha katika uso wa dunia naona umechoka kuishi
Jesca huku akilia kwa kwikwi alisema
``mama shushu kumbuka Mungu yupo unataka niue kichanga kilichotumboni mwangu ,kichanga hakina kosa lolote nakwambia mama ukitaka niue sipo tayari kuua kichanga hiki’’
Alipotamka maneno haya hadi waliokuwa pale pembeni waliogopa ,walijikuta wakipiga magoti chini na kusema
``mama shushu tunakuomba umsamehe tuu huyu hajui anachokisema ‘’
Mama shushu alicheka sana kwa kejeli
``wewe mbwa tena hii mimba wenda ulibakwa leo wajikuta unataka kuibeba sasa leo wewe na kijusi chako huko tumboni mnakufa wote pumbavu zenu’’
Mama shushu alitoka nje
Wafanyakazi wale kwa hofu walimsihi sana jesca
``wewe mwanamke ndio unakufa hivyo wacha kulumbana na mama chuchu utakufa sasa hivi hanaga mawili huyu mama;;’’
Jesca aliwajibu
``mimi siwezi kuua kichanga pia siwezi kulala na mwanaume yoyote katika kambi hii full stop’’
Wafanyakazi wale waliona sasa jesca ameamua kufa mwenyewe walimwacha mwenyewe
Mama shushu alitoka nje kwa hasira alipitiliza hadi chumbani kwake alichukua bastola yake ambayo alishawahi kuua nayo zaidi ya wanawake 100 alirudi kuelekea alipo jesca alijisemea moyoni
``huyu msichana sasa dharau alizokwisha nifanyia zinatosha leo namuua kabisa ‘’
Akiwa anaelekea ,bibi mmoja alipiga magoti chini na kusema
``mama shushu mama usimwage damu tafadhali naomba nikupe njia sahihi mama ‘’
Mama shushu alimpiga bibi Yule kikumbo na kusogea mbele ,bibi Yule alilia kwa sauti
``mama shushu nimekua mfanyakazi wako wa muda mrefu nisikie tafadhali’’
Mama shushu taratibu maneno yale yalimwingia masikioni alirudi nyuma na kumwambia bibi Yule
``nini unataka kusema kama niupuuzi nakufyatua na wewe mshenzi kabisa wewe’’
``samahani mwanangu unaonaje ukanipa kazi yakutoa mimba ya huyu kwa kutumia sumu ,tunaweka kwenye chakula akila inatoka ndani ya dakika tano,,huyu binti ni mrembo utapoteza hela nyingi sana ‘’
Mama shushu aliachia tabasamu
``hahaha ndio maana nakupendaga bibi sasa fanya kazi hii mchana huu kila kitu kiwe sawa nadhani wewe wafahamu ukishindwa kazi nini kinafuata’’
Bibi alipewa kazi hiyo kwa haraka alipitiliza ndani ya chumba chake cha kazi ,alitoka na sumu ile maalumu kwa ajili ya kutolea mimba ,sumu hiyo ilikua na uwezo wa ajabu sana ilikua ikikatakata kichanga na ndani ya dakika zisizozidi tano kichanga kinakufa na kutoka
Alipomaliza kuandaa sumu ile alitilia kwenye chakula cha jesca cha mchana
Upande wa pili vijana wa mama shushu mchana ule walikua wamevamia mitaa ya matajiri kwa ajili ya kuteka watoto ili wawafanye makahaba ,kwa mbali waliona msichana mzuri sana akiwa na kaka yake wakiwa wanacheza magemu ndani ya geti la nyumba yao ,watoto hao walikuwa ni watoto wakishua walikuwa ni matajiri sana
Masoya kijana wa mama shushu alituliza gari na kuzama ndani ya uzio alichokifanya alipowakaribia watoto wale alimwasha mtoto Yule wa kiume bastola ya kichwa na kumdaka Yule wa kike ,alimziba mdomo ili asipige kelele
Mtoto yulen wa kiume alifia pale pale walimkamata dada yake tayari kwa ajili ya kumpeleka kwa mama shushu
Msichana Yule alilia sana kwani alishuhudia kifo cha kaka yake ,pia hakujua wapi anapelekwa
Mzee derrick baba wa watoto wale alitoka nje kwa furaha akisema
``woooooo my son and daughter nipo na zawadiiii njooni wanangu ‘’
Mzee derrick alishangaa wanae wapo kimya aliingiwa na hofu wala kelele zao hazikusiskika
Alipotoka nje na kuangalia kwenye majani ya ukoka alikuta simu zenye magemu zipo chini ,taratibu alisogea ,,,mzee Yule alichokiona miguu iliishiwa nguvu ,kijana ake wa pekee wa kiume alikua chini kichwa chake kikiwa kimepasuliwa na risasi
Mzee Yule alipiga kelele ``MUngu wanguuuu eee kwanini umeruhusu hili ‘’
Dakika mbili watu walifurika pale ,mama yao na watoto wale alipofika pale alizimia hapo hapo
Upande mwingine jesca aliitwa na bibi tayari kwa ajili ya kula chakula
Jesca alisogelea meza akashika kijiko chake kwa matamanio makubwa ya kula kwani toka asubuhi hakuwa amekula
Je nini kitaendeleaaaa
Jesca atapona ,kwa bintialiyetekwa je fuatilia zaidi

No comments