NAJUTA KUZALIWA MWANAMKE 07
Hussein alimshukuru sana jesca , muda wote jesca akiwa anaongea Hussein alimtazama tu usoni alijikuta akivutiwa sana na yule binti Hussein alitamani amweleze jesca kilichoujaza moyo
Jesca nae alihisi kitu kwa mshangao aliuliza
``kaka husssein mbona waduwaa’’
Hussein alivunja ukimya alimweleza kila kitu jesca alimwambia jesca ikiwezekana wakaishi wote ,Hussein alimweleza jesca historia yote na kila kitu kuhusu maisha yake
Jesca alijikuta akikubali kwani aliyofanyiwa na dokta ni mengi mno hakuwa na cha kulipa
Hussein alifurahi mno kukubaliwa ombi lake na jesca alimshika jesca na kumkumbatia kwa furaha ,wakiwa wanakumbatiana ghafla nesi subira aliingia
Jesca alimsalimu kwa furaha hali kadhalika Hussein alimsalimu
Cha kushangaza subira hakujibu alitupa faili kwenye meza ya Hussein kisha alitoka nje
Subira alipitiliza hadi nje chini ya mti wa kivuli aliuma mdomo kwa hasira
``huyu dokta Hussein kumbe kumtunza huyu binti na kumtibu kote kumbe alikua akimtaka kimapenzi ,,,Mungu wangu sasa mimi kila siku namendea nyuma ni kuwa dokta anipendi au daaah huyu mporipori asiye na kwao anapendwa na dokta haaaa’
Subira alichukia sana aliingia maabara na kuchukua sindano yenye sumu alipanga kuwa ikifika muda wa kumchoma jesca sindano ya kukausha vidonda lazima amchome sindano yenye sumu ili amuue kabisa asije mwachia nafasi ya kumchukua Hussein
Ilipofika saa mbili usiku ,jesca akiwa kitandani huku akiwa na furaha tele ,aliwaza sana juu ya maisha yake ,hakuamini kama atakuwa mke wa dokta alimsukuru Mungu sana aliamini ,maneno ya Mungu kuwa ``mungu anaweza kumtoa mtu mavumbini na kumketisha palipotukuka
Akiwa anawaza hivyo ,nesi subira aliingia akiwa ameshikilia vifaa vyake vya kazi ,sindano na dawa
Subira alipofika kitandani mwa jesca alimsalimu jesca salamu ya kinafiki
``vipi my unaendeleaje ,naomba tumalizie sindano ya mwisho naona hali yako kwa sasa ni nzuri’’
Jesca alipandisha nguo yake kwa ajili ya kuchomwa sindano
Nesi subira katika maisha yake hajawahi kuua hata siku moja ,ila kutokana na wivu wa mapenzi leo kwa mara ya kwanza anakwenda kuua
Nesi subira aliinua sindano yake juu ,sindano ilikua ikitoa povu kwani sumu iliyokuwa ndani ilikua ni hatari sana ,,,subira alipokuwa akishusha mkono ili achome sindano ,kwa haraka alikumbuka kamera za hospitali zipo wazi ,aligundua zisipozimwa lazima wakifuatili chanzo cha kifo na yeye atahusishwa kwenye hili ,kwa haraka aliweka sindano chini na kuanza kuondoka
Jesca alimwambia subira ``nesi leo kuna nini naona unajishauri kunidunga nishazoea mama usinionee huruma bwana ‘’
``hahaha usijali mama naja kukuchoma sasa hivi nimesahau kitu nakuja jifunike kwanza nakuja ‘’
Jesca alishusha nguo yake aliyokuwa amepandisha ,subira aliondoka hadi ofisi kuu kwa ajili ya kuzima kamera zote za upelelezi (cctv camera) alipozima alianza kurejea alipo jesca
Upande wa pili dokta Hussein akiwa ofisini alishtushwa sana na kuzimwa kwa kamera ,ofisini mwa Hussein kulikua na kamera moja iliyoungwa kila mara iliwasha kitaa hivyo kitendo cha kamera kuzimwa kitaa kilizima ,,Hussein alijua lazima kuna uhasama unataka kufanywa hospitalini pale ,kwa haraka mtu wa kwanza kumwaza ni jesca ,dokta Hussein alitokea kumpenda sana jesca ,,alikimbia hadi wodi aliyokuwamo jesca ,alipofika ndani alikuta vifaa sindano pamoja na dawa zipo mezani na jesca yupo kitandani
Hussein alijiuliza maswali ``mhhhhh subira ndio yupo zamu kaenda wapi atakuja kutuulia mgonjwa hadi sasa hivi hajamchoma ‘’
Dokta Hussein alichukua sindano na kuishika ili amchome jesca kwa niaba kwani alihofia muda kuenda
Alipoishika sindano alishtushwa sana kuona ikiwa inachemka huku ikitoa mapovu ya kutosha ,husein kwa haraka aliichukua na kukimbia ,maabara kwa ajili ya vipimo ,alipoipima aligundua ina sumu aina ya dotrodiux ,hii ni sumu kali ambayo inaua ndani ya sekunde chache ,,,,Hussein aliishiwa nguvu alijisemea
``duuuuuh subira leo unataka kumuua jesca ,,kweli moyo wa mwanadamu kichaka ‘’
Hussein alikimbia haraka wodini na kuketi pembeni ya meza
Subira njiani alikuja haraka kutimiza azma yake alipoingia ndani ya wodi ile aligongana ana kwa ana na Hussein
Alipotazama mezani hapakuwa na dawa wala sindano ,,,,,,,subira alidondoka chini na kuzimia ,,alijua leo kibarua hana ,Hussein toka azaliwe hajawahi tetea uovu hata umhonge akubali anasimamia ukweli ,je kwa mtu anayempenda kama jesca
Baada ya kuzinduka subira alipigwa pingu na kupelekwa ndani kesi yake wala haikuwa na dhamana kwani ilikua ni uuaji wa wazi wazi ,baadhi ya pakitin za sumu zilipatikana katika droo yake hivyo hakuwa na lakujitetea kabisa
BAADA YA WIKI TATU
Jesca na Hussein mapenzi yao yalikuwa na kushamiri ,mapenzi yao yalizua stori mpya katika hospitali ile kila mfanyakazi alikua akimbeza sana Hussein wengi walimkejeli na kumwambia
``wewe mpuuzi sana wewe yaan unataka kuoa mwanamke asiye na kwao kweli wewe umechezewa wewe ‘’
Hussein hakusikiliza maneno yao ,,hatimaye alimchukua jesca rasmi kabisa ,alifanya sherehe ndogo iliyohusisha marafiki zake wa karibu ,watu walikuja ,ndugu zake na Hussein walikuja ,ilikua ni sherehe ndogo yenye raha yake
Hussein alipopewa muda wa kuzungumza alisimama na kusema
``jamani sina mengi ya kusema ila huyu binti naona ni mtu sahihi Mungu amepanga niwe nae ,nampenda sana na nitamtunza milele’’ watu walipiga kelele na kushangilia kwa nguvu ishara yak umpongeza
Baada ya dakika mbili jesca nae alisimamishwa
``kwanza kabisa namshukru Mungu pili namshukuru Hussein kwa kunifanya kuwa mke wake bila kujali mapungufu yangu zipo zaidi ya sababu elfu za kuniacha ila yeye amenipenda asante hussien pia nashukuru wazazi wake na marafiki wote mliokusanyika hapa ‘’
Jesca alikaa ,watu waliushangilia ila baadhi ya rafiki za husseinakina aisha na grace walikua wakifinyana ``shogaaa jamaniii huyu Hussein hakukuona hata wewe anaenda kumchukua huyu mpori pori khaaaa’’
Sherehe ilikwisha kila mmoja aliondoka kwao ,jesca alibaki na mpenzi wake Hussein ,hakika Hussein alikua amejiendeleza sana nyumbani kwake kulikua kama ulaya ,nyumba ilikua ni ya kisasa sebule usiseme masofa jikoni ,jiko la umeme ,,,,,,,kila mahali palikua panavutia
Jesca alitoka katika umaskini na kuamkia utajiri
Siku hiyo jesca alijivinjari na hussein ,,,,,waliburudika sana,waswahili husema
``mapenzi matamu ni yale yanayotoka kwa wapendanao wanopendana kutoka moyoni’’
Hussein alimshika mkewe na kumkumbatia kwa nguvu huku akiimnong’oneza
``mke wangu mtoto wetu akizaliwa tutamwita happy ,,,,yaan furaha maana kweli leo tumekua na furaha na amani sawa mke wangu’’
Jesca alimkiss Hussein shavuni na kumwambia ``usijali kipenzi changu tutafanya hivyo’’
Waliburudika sana usiku huo kila mmoja alilala akiwa na furaha ,jesca alikilalia kifua cha Hussein ,hakika alijihisi kama malaika ,hakuamini kama atapata amani kama hii duniani ,,,,kilichomfurahisha zaidi ni ahadi Hussein aliyompa ya kuwatafuta wazazi na familia yake ,jesca alisikia raha sana
Ilipofika kesho yake siku ya jumamosi walichukuana na kutembelea maeneo mbalimbali wakiwa na gari lao ,walivinjari kupita maelezo ,,,ilifika hatua jesca alitokwa na machozi ya furaha ,,,husein alichukua kitambaa na kumfuta huku akimwambia
``wewe ndio ,malaika wa moyo wangu unastahili wala usilie ‘’
Wikiend ilikwenda vyema kila kitu kilikua sawa kila mmoja alimfurahia mwenzake
Jumatatu asubuhi jesca aliamka asubuhi na mapema alimwandalia mume wake chai maji ya kuoga na nguo baada ya Hussein kuoga kila kitu kilikua sawa alivalishwa vyema kisha alichukua gari lake na kwenda kazini
Hussein akiwa njiani mbele yake aliona watoto wawili wakiwa wanacheza barabarani ,Hussein alipiga honi kuwataka waondoke ila watoto wale waliendelea kutanga tanga wasijue wanaenda wapi
Hussen alijitahidi kuwakwepa kwa kila namna ila alishindwa ,gari la Hussein liliwavaa watoto wale na kuwasagasaga ,kisha lilipinduka mara tatu ,si husseinsi watoto wote walikufa
Watu walikimbilia mahali pale ,wasamaria wema walijitahidi kuwasaidia ila huwezi amini Hussein alipoteza maisha pale pale ,,,,,,pembeni ya gari simu ya Hussein ilionekana baba mmoja aliichukua ,kwa haraka aliona namba imeseviwa MKE WANGU’’ waliichukua na kupiga simu , kwa bahati nzuri simu iliita
Jesca akiwa ndani anafanya usafi aliona simu yake ikiita ,alivyoona jina MUME WANGU aliachia tabasamu la nguvu
Je nini kitaendeleaaaaaa
Share simulizi hii tuendelee
No comments