MUFTI WA TANZANIA AAGIZA KUFUNGWA KWA MADRASA ZOTE
Mufti wa Tanzania, Sheikh Aboubakar Zubeir ameagiza madrasa zote nchini kufungwa kuanzia leo Jumatano Machi 18, ili kupunguza ongezeko la maambukizi ya ugonjwa wa corona.
Akizungumza leo Jumatano Machi 18, jijini Dar es Salaam Sheikh Zubeir amesema agizo hilo linapaswa kutekelezwa haraka iwezekanavyo na kwamba taarifa zaidi zitaendelea kutolewa.
Amesema kuhusu Swala ya Ijumaa na ile ya Jamaa zitaruhusiwa kwa sasa na huenda itabadilishwa kulingana na mazingira ya ugonjwa huo.
“Kuanzia sasa swala za Jamaa zinapaswa kuswaliwa kwa kuachiana nafasi na kuzingatia usafi ili kupunguza maambukizi,” amesema Sheikh Zubeir.
Amesema kwa maeneo ambayo yanawashukiwa wa ugonjwa huo na yamewekwa karantini hairuhusiwi kuendelea na swala hizo kwani hata vitabu vya dini vinaelekeza kuwa ni dhambi kumuambukiza ugonjwa mwenzio kwa makusudi,” amesema.
Amesema muislamu yeyote atakayepata na maradhi haya ni haramu kwake kuhudhuria swala za Ijumaa na Jamaa kama ambavyo ni haramu kwake kuchanganyika na wengine kwani kufanya hivyo ni kuisambaza na kueneza ugonjwa huo kwa wenzake.g
Casino Nightclub - Mapyro
ReplyDeleteCasino Nightclub is located on 37th floor at 여주 출장마사지 3600 West Flamingo Road, Suite 삼척 출장안마 104, USA. The property is owned and operated by Treasure 구리 출장마사지 Island 남양주 출장샵 Hotel & Casino, 안양 출장샵 LLC,