NAJUTA KUZALIWA MWANAMKE 05


NAJUTA KUZALIWA MWANAMKE 5

Mama kenedy alisogea pembeni na kuchukua pasi ya umeme iliyokuwa pembeni aliongeza moto hadi mwisho ,alimkokota jesca hadi ilipo pasi
Jesca alipambana huku akisema ``mama kenedy niamini shida ni  huyu bwana wako siyo mimi hata Mungu anaona ‘’
Mama kenedy wazimu wake ukimpanda anakuwa na nguvu kama simba alimzaba jesca  kibao kimoja
Jesca alidondoka hadi chini kwenye kapeti
Mama kenedy alichomoa pasi kwenye moto ,alimvua jesca  nguo za juu ,bila huruma alipitisha pasi ya moto mgongoni mwa jesca
Jesca alipiga kelele moja kubwa sana iliyoambatana na uchungu wa hali ya juu ,sauti aliyotoa jesca iliwavuta  majirani ,mlinzi na wapitia njia kuja kushuhudia nini kinafanyika
Mama kenedy bila huruma aliendelea kumchoma jesca na pasi maumivu yalikua makali hadi jesca alizimia
Ndani ya dakika chache umati wa watu ulikusanyika ,baba kenedy alikua nje akiwazuia wasiingie
Baadhi ya majirani walifanya fujo na kuzama ndani ya nyumba kushuhudia kuna ni? Kwani hali ilikua ni tete mno isivyo kawaida ,kila mtu aliyefika sebuleni pale machozi yalimtoka ,hadi kina baba walijikuta wakilia kwa uchungu sana,mgongo wa jesca ulikua umechomwa chomwa ,mafuta yaliyochanganyika na damu yalionekana juu ya mgongo wake ,mzee mmoja alisema
``jamani huu sio ubinadamu hebu fikiria tu maumivu unayoyasikia pale unapochoma kakidole kwa moto ,hebu haraka huyu apelekwe hospitalini’’
Wanawake walikua wakikazana kumpepea jesca wengine wakimnyizia dawa ya unga unga kupunguza maumivu’’
Mama kenedy badala ya kutulia alianza kuropoka
``mwacheni huyu kahaba asiye na kwao mwizi wa waume za watu  huyu’’
Mzee yusuph alimpiga mama kenedy kofi kubwa ``paaaaaaaaah !!!!!!!!!!!!! mpumbavu wewe nakwambia  Mungu lazima akulipe kwa haya uliyoyafanya shenzi type ‘’
Baba kenedy alipoona majirani wamechafukwa alitoa gari yake nje na kushirikiana na baadhi ya majirani kumwingiza jesca kwa gari ,jesca likua akihisi maumivu makali ,walivyokuwa wakimbeba mgongo mzima ulikua ukiwaka moto alisikia maumivu kupindukia ,ama kweli maumivu ya moto siyo ya kitoto.
Jesca alipowekwa ndani ya gari majirani walimwacha na kuondoka zao kwani walijua sasa usalama wa jesca utapatikana ,mama kenedy huku akikunja mdomo kama konokono alipanda ndani ya gari yeye na bwana wake kumpeleka jesca hospitalini
Ilikua ni saa nne usiku kwa upande wa majira ,mama kenedy alimwuliza mumewe
``huyu kahaba wako tumpeleke serena hospital ama mdalaksi dispensary ‘’
``kanusha kauli yako weee mimi si husiki huyu msichana mchafu sana ulivyoondoka alisimama na kuanza kunitega mwenyewe wala siyo mimi nimemwomba ‘’’
Mama kenedy alisikia hasira sana alimgeuzia macho jesca aliyekua akilia kwa maumivu ,kikubwa sana kilicho mliza jesca ni jinsi ambavyo baba kenedy alivyomruka ,jesca alikumbuka maneno ya mama yake ``wanaume siyo watu wakishakutumia wanakutupa kama maganda ya muwa ‘’
Mama kenedy alimwambia jesca kwa ukali
``wewe kahaba natamani hata ukafe tu huna sababu ya kuishi humu duniani ‘’
Jesca alijibu huku akilia kwa uchungu
``Mungu yupo nasema yupo atanisimamia na nyie pia atawalipa sawasawa na mlivyo tenda tena Mungu achelewi ,nasema Mungu yupo ‘’
Mama kenedy alicheka kwa dharau
``hahahahah mjinga kabisa wewe toka lini Mungu akasikia kilio cha makahaba,wezi wa waume za watu nakwambia wewe hizo ni kelele za chura’’
Ndani ya lisaa waliwasili hospitali kubwa ya serena ,walipofika waliona milango imefungwa
Baba kenedy alisema
``hivi mama kenedy my sweet nikupendae ,waonaje huyu kahaba tumwache hapa nje ya geti lazima watamsaidia tu hamna jinsi ‘’
``ohooooo sweet wazoooo  zuri kabisa honey tena mimi nilitaka tumtupe kwenye korongo kule afe kabisa maana hastahili kuishi’’

Mama kenedy na baba kenedy alimshika jesca mithili ya mtu anayekokota kiroba cha mahindi na kumtupa nje ya geti la hospitali ,,,,
Jesca hakuamini alichokiona  ,alitupwa chini kisha walipanda ndani ya gari na kuondoka
Jesca alipigwa baridi ,alikua akiumwa maumivu yasiyoelezeka ,alikua hawezi hata kunyanyuka kwani mgongo ulikua na vidonda vya kutosha alilala kwenye mchanga na tumbo kwani alihofia kuvitonesha vidonda vyake hivyo,,………..
Walinzi wageti la hospitali walikua geti la chini geti la juu waliwaacha mbwa wakizungu ambao ni walinzi ,,,,mbwa mmoja alinusa na kubaini kuna hali isiyo ya kawaida alipiga kelele na kukimbilia nje ya geti alipomwona jesca alibweka mara moja kisha alitoka spidi hadi ndani ya ofisi ya daktari wazamu ,mbwa wakizungu wamefunzwa sana ,wana akili kupindukia wanaweza kueleza hali halisi ilivyo ,mbwa alifika mbele ya dokta na kujigaragaza chini huku akizunguka nakuonyesha jinsi jesca alivyokuwa pale chini ,,,dokta nae alikua na saikolojia kubwa aligundua kuna mtu anatatizo kwa haraka aliongozana na mbwa hadi nje ya geti ,,,,hakika Mungu akitaka kukusaidia anaweza kutumia chochote kama wanadamu wameshindwa hadi mbwa anaweza kukusaidia
Dokta alipomwona jesca alichuchumaa chini na kumwoji maswali ,jesca alijibu kwa kujing’ata ng’ata kwani alikua akiumwa kupita maelezo
``jamani umefanya nini binti mrembo kama wewe,ohooo my God nani kakuchoma khaaa kweli wanadamu wana  roho mbaya sana ‘’
Dokta alitokwa na machozi kama mvua baada ya kuona vidonda vya jesca ,aliinama na kumnong’onezea  ``usijali nitakuwa pamoja na wewe hadi upone sawa’’
``asante kaka nashukuru ‘’
Jesca alipata matumaini kwa maneno ya dokta Yule aliyeonekana mpole na mtaratibu
Jesca alichukuliwa na kupelekwa kwenye chumba cha wagonjwa mahutihuti kwa ajili matibabu ya haraka
Upande wa pili baba kenedy alikimbiza gari huku akiwa anacheka sana na mkewe
Walipofika mbele kidogo kwenye kilima kirefu ,gari lao liliacha njia na kuanza kuserereka ,mama kenedy alipiga kelele kubwa
``baba kenedy shika breki mpuzi wewe tutakufa eti ‘’
Baba kene alishika breki ,huwezi amini breki zilikataa katakata ,,gari iliendelea kuserereka
Mama kenedy alisema ``baba kene gari likidumbukia kwa korongo lile hatuponi’’
Kabla hajamalizi sentensi gari lilibinuka mara tatu hadi korongoni ‘’
Baba kenedy alipoteza maisha pale pale ,mama kenedy alikatika katika mikono na miguu ‘’
Kwa haraka watu waliwasili pale na kumchukua mama kenedy kumwaisha serena hospital
Baba kenedy alipelekwa moja kwa moja mochwari kwani  alikua ni marehemu ,mama kenedy aliwahishwa chumba cha wagonjwa mahutihuti
Jesca akiwa kitandani anafanyiwa matibabu alisikia madaktari wakisemezana
``jamani kazaneni kuna ajali imetokea mmoja kafa ila mama ni mahutihuti kaletwa humu ,,,hali yake ni mbaya ‘’
``daaah ni ajali ya nini hii ‘’
``ya gari limepindukia hapo kwenye korongo la muleba bar’’
``daaah ‘’
Jesca alishtuka sana alijisemea
``Mungu wangu usikute ni mama kenedy na baba kenedy tu ,,,,Mungu epusha hawastahili kupata adhabu hiyo mbaya namna hii’’
Jesca akiwa kitandani dokta alimuuliza
``jesca mbona kama umeshtuka ‘’
Kabla jesca hajajibu alimwona mama kenedy akiingizwa chumba cha mahutihuti akiwa juu ya machela
Je nini kitaendeleaaa


No comments

Theme images by jangeltun. Powered by Blogger.